YOU ARE IN GOOD HAND WITH OUR COMPANY

ENJOY OUR SERVICE DAILY...............

CALL: +255765257825

WE ARE NOW SHINYANGA......

PRAY HARD AND WORK HARD

DON'T MISS, MAKE YOUR LIFE BETTER VIA TDIS.....

INFORMATION TECHNOLOGY is no 1

HELPS YOUR BUSINESS...........

Wednesday, October 14, 2015

JK aitaka Tanesco kuchangamkia fursa

RAIS Jakaya Kikwete amezindua kituo cha kufua umeme kwa mitambo ya gesi asilia cha Kinyerezi I na kutaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuchangamkia fursa ya upungufu wa umeme Afrika ili kuwa na uhakika wa mapato. Alisema duniani umeme unaozalishwa ni megawati milioni 5,255,000 na mataifa makubwa matano yanazalisha asilimia 55 wa megawati hizo, ambayo ni China inaongoza kwa megawati milioni 1,146,000, Marekani milioni 139,000, Japan 287,000, Urusi 223,000 na India 280,000. Alisema megawati zinazobakia, ndiyo nchi nyingine 193 zinazotambulika na Umoja wa Mataifa wanagawana, ambapo Afrika zinazalishwa megawati 111,786, idadi ambayo hata nusu ya India haifikii. Alisema Afrika Kusini wanaongoza kwa kuzalisha megawati 44,260, Misri megawati 26,910, Algeria megawati 11,330, Libya megawati 6,763, Morocco megawati 6,620 na Nigeria megawati 5,600. Rais Kikwete alisema katika nchi za Afrika Mashariki, Kenya inaongoza kwa megawati 2,465, Tanzania 1,498, Uganda megawati 850, Rwanda megawati 110 na Burundi megawati 53, hali inayoonesha kuna tatizo kubwa la upatikanaji wa umeme. “Lakini kwa kuwa nchi yetu imejaliwa vyanzo vingi vya nishati ni fursa na kugeuza kuwa biashara, kwani Kenya wanahitaji megawati 1,000, Rwanda, Zambia na wengineo wanataka kwa haraka huku wengine wakitaka kujenga bomba la kupeleka gesi wenyewe,” alisema. Alisema kwa sasa nchi inapita kwenye changamoto, kwani umeme wa maji unaingiza megawati 561 katika gridi ya taifa, lakini sasa zinazoingia ni megawati 105 na upungufu ni megawati 450. Alisema alitegemea kutakuwa na vituo zaidi kuzalisha umeme, kwani bomba lina uwezo wa kusafirisha gesi kutengeneza megawati 3,000, lakini bado kuna nafasi kufikia malengo kwa kujenga haraka vituo vingine. Alisema katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano unaokamilika mwakani mwishoni, lengo ni kufikisha megawati 2,780, lakini sasa kuna megawati 1,490, hivyo kudaiwa megawati 1,390. Alisisitiza kwamba jitihada zinahitajika kufikisha hizo mwakani. Alisema baada ya kukamilika Kinyerezi I, mwezi ujao itakamilika Kinyerezi II na Januari mwakani Kinyerezi III, hivyo ni lazima kuongeza kasi. Kikwete aliwataka Tanesco kuongeza kasi ili kuchangamkia fursa na kuingiza umeme haraka na kupunguza mgao uliopo sasa. Alisisitiza shirika hilo la umeme kuzingatia sheria ya manunuzi kwa umma. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Ngosi Mwihava alisema katika utawala wa Rais Jakaya Kikwete, vituo vya kufua umeme vya megawati 484.8 vimejengwa na pia asilimia 47 ya mitambo ya kufua umeme imejengwa . Alisema, miradi mingi ya kufua, kusafirisha na kusambaza umeme inaendelea na ujenzi. Alisema tangu Septemba 17 mwaka huu, walipoanza kuwasha mitambo ya gesi asilia, wameongeza megawati 200 ambazo hazikuwepo kabla ya gesi kuanza kusafirishwa, vinginevyo hali ingekuwa mbaya zaidi, kwani kungekuwa na ukosefu wa megawati 400. Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba alisema kituo hicho kimoja, kati ya vinne vinavyojengwa, vikikamilika , vina uwezo wa kutoa megawati 1,500. Kituo cha Kinyerezi I kimegharimu Sh bilioni 400. “Kwa sasa mitambo miwili yenye uwezo wa kuzalisha megawati 70 ndiyo imeishajaribiwa na tayari inazalisha umeme na miwili iliyobaki ina jumla ya megawati 80 itaanza kujaribiwa na itakamilishwa na kuunganishwa mwisho wa mwezi huu,” alisema.

‘Sitakubali viongozi walalamikaji’

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli amesema hayupo tayari kuona viongozi wakigeuka kuwa walalamikaji. Badala yake, amesema viongozi hao watabanwa, wachukue hatua na uamuzi mgumu kwa maslahi ya taifa na wananchi wake. Magufuli ameahidi kukomesha mapigano na mauaji baina ya wafugaji na wakulima kwa kusimamia haki za kila kundi kikamilifu. Aidha, amesema ataweka mfumo mpya wa utoaji wa ruzuku za dawa za mifugo na pia kutoa dawa kwa wafugaji na kuchimba mabwawa ya kunywesha na kuosha mifugo. Alisema hayo alipozungumza na wakazi wa miji mbalimbali ya Mkoa wa Pwani akiwa katika ziara ya kampeni kwa mkoa huo. Baadaye alifanya mkutano mkubwa wa hadhara katika mji wa Mkuranga. Kuhusu viongozi kuchukua hatua badala ya kulalamika, Dk Magufuli alisema katika uongozi wake, kamwe hataunda serikali ya viongoziwalalamikaji, badala yake wanaochukua hatua kwa malalamiko ya wananchi. “Sitakubali wafanyabiashara walalamike, wakulima walalamike, wafugaji walalamike, wavuvi walalamike; halafu eti na viongozi wanalalamika. Sasa kiongozi ukilalamika, nani achukue hatua na uamuzi mgumu kama sio kiongozi ili kumaliza malalamiko ya wananchi?” alihoji Dk Magufuli. Alisema akiwa Waziri wa Ujenzi, alikuwa analala katika makambi mbalimbali kusimamia ujenzi wa barabara na madaraja, hivyo atapenda kuwaona mawaziri atakaowateua washinde na kulala katika miradi ya sekta zao ili kulifanya taifa kupata mabadiliko ya haraka kwa maendeleo ya wananchi. “Kama mimi nililala barabarani wakati wa kujenga barabara hii (Dar- Mtwara- Tunduru), ole wake Waziri wa Ujenzi nitakayemteua afanye kazi kwa kushinda ofisini. Mimi mawaziri wa ofisini hawana nafasi, mtu wa aina hiyo ni bora nikimteua akatae. “Kama ni Waziri wa Elimu akeshe kuinua elimu, kama ni wa Miundombinu akeshe kwenye miundombinu, kama ni wa afya akeshe kwenye afya, kama ni wa maji akeshe kwenye maji. Kamwe sitakubali Waziri wa kuja kurudisha nyuma azma yangu ya kuwafanyia kazi Watanzania. Kwangu mimi ni Kazi Tu,” alisema. Kuhusu kukomesha mauaji baina ya wafugaji na wakulima, Dk Magufuli alisema atasimamia kuundwa sheria mpya, zitakazosimamia kilimo na ufugaji ili kuanisha haki na mipaka kwa kila kundi ili kufanya makundi hayo yasiingiliane, hatua ambayo imekuwa chanzo cha mapigano na mauaji. “Ni lazima wafugaji waheshimu wakulima na wakulima ni lazima waheshimu wafugaji, lakini pia wakulima na wafugaji ni lazima waheshimu wavuvi. Serikali yangu itatambua na kuheshimu kila kundi kisheria. Mimi ni mtoto wa mkulima na mfugaji hivyo natambua nini nifanye ili kuboresha makundi haya,” alisema. Alisema kwa muda mrefu sasa, taifa limekuwa likishuhudia matukio ya mauaji baina ya wakulima na wafugaji na kwamba hali hiyo haiwezi kuachwa ikaendelea kutokea, kwa vile licha ya kusababisha hasara kwa mali za wakulima na wafugaji, pia husababisha mauaji kwa watu wasio na hatia. Aidha, mgombea huyo alisema katika uongozi wake, atamwaga mikopo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi ili waweze kuongeza mitaji na kuendesha shughuli zao kwa lengo la kukuza pato lao na pato la taifa na hivyo kusukuma maendeleo ya taifa. “Watu wamechoka na umasikini, wanahitaji ukombozi na mtu muafaka kwa Tanzania mpya na ya maendeleo ya kasi ni Dk Magufuli, hivyo nawaomba mnichague,” alisema Dk Magufuli. Akiwa Kibiti, aliahidi kuboresha miundombinu ya barabara, maji na kujengwa kwa hospitali ya kisasa itakayokuwa na uwezo wa kupima magonjwa mbalimbali, lakini pia kusaidia katika ujenzi wa mji wa Kibiti baada ya kupandishwa hadhi kuwa wilaya. Akiwa wilayani Kilwa mkoani Lindi mapema jana, Dk Magufuli aliahidi kuubadili mji wa Kilwa Masoko ili kuufanya kuwa kitovu cha utalii kwa lengo la kuongeza thamani ya maisha na bidhaa katika wilaya hiyo, yenye utajiriwa kihistoria nchini. Pamoja na kuhutubia wakazi katika miji mikubwa, Dk Magufuli amekuwa akisimama na kufanya mikutano midogo katika vijiji mbalimbali vya wilaya, hatua ambayo imekuwa ikimwezesha kukutana na wapigakura wengi wa maeneo ya vijijini.

Wanajeshi wastaafu wakerwa na Ukawa

WANAJESHI wastaafu nchini wamevitaka vyama vinavyounda umoja wa Ukawa kufuta usemi wake kwamba wapo wanajeshi wastaafu waliojiunga nao kwa ajili ya kusaidia mikakati ya kufanikisha ushindi wao. Walitoa kauli hiyo kwenye kikao cha pamoja baina ya wanajeshi hao wastaafu na viongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) uliokuwa ukilenga kutoa elimu na hamasa kwa wanajeshi hao wastaafu kujiunga na huduma za matibabu za mfuko huo. Wakizungumza katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa NSSF mjini Kigoma, wanajeshi hao wastaafu wamesema kuwa kauli ya Ukawa imewadhalilisha na wametaka kuombwa radhi kwa hilo. Mwenyekiti wa Muungano wa Wanajeshi wastaafu nchini (Muwawata), Assedy Mayugi alisema madai kwamba wapo wanajeshi wastaafu 200 kila mkoa waliojiunga na umoja huo ni upotoshaji kwa umma. Akisoma tamko kwa niaba ya wanajeshi wastaafu wa mkoa Kigoma, Kibwana Shomari alisema wanajeshi wastaafu wa mkoa Kigoma bado watiifu kwa Amiri Jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali iliyopo madarakani. “Kiapo tulichokula cha kuwa watiifu kwa amri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi ya wananchi wa Tanzania na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tunaendelea kuwa watiifu kwa serikali iliyopo madarakani,” alisema. Akizungumzia huduma za matibabu zinazotolewa na mfuko huo, Meneja wa NSSF mkoa Kigoma, Josephat Komba alisema wanajeshi hao wanayo fursa nzuri ya kujiunga na huduma hiyo na kupata matibabu katika kiwango knachostahili. Komba alisema wanajeshi hao wastaafu wakijiunga na huduma za matibabu za mfuko kwa kuchangia kila mwezi, watapata matibabu na wategemezi wao.

NEC kutumia mfumo mpya

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jji Mstaafu, Damian Lubuva akizungumza na wanahabari juu ya mambo yahusuyo tume hiyo. TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kutumia mfumo mpya wa kielektroniki katika kujumlisha matokeo ya kura kwa lengo la kuondoa makosa mbalimbali ya kibinadamu, yanayoweza kutokea kwa bahati mbaya wakati wa kujumlisha matokeo hayo katika uchaguzi mkuu. Mfumo huo mpya wa Menejimenti ya Matokeo (RMS), unatumia mashine za kisasa zenye uwezo wa kuchapisha na kunukushi karatasi za kupigia kura zaidi ya 60 kwa dakika moja. Mkurugenzi wa NEC, Kailima Kombwey alisema jana kwamba Oktoba 11, mwaka huu, waliwaalika wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) kutoka vyama vyote vya siasa na mfumo huo ukapitishwa. Akiwasilisha mada ya maandalizi ya uchaguzi, Kombwey alitaja makosa yanayoweza kutokea katika kujumlisha kura ni pamoja na matokeo ya kituo kimoja, kujumlishwa zaidi ya mara mbili, kukosea uandikaji wa namba na usahihi wa ujumlishaji. “Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 mfumo huu ulisanifiwa upya na kutumika, hata hivyo kasoro chache zilioneshwa. Kwa uchaguzi wa mwaka huu, tume imeboresha mfumo huu na kuondoa upungufu katika maeneo yote yaliyokuwa na changamoto mwaka 2010,” alisisitiza Kombwey. Alisema pamoja na mfumo huo, pia tume hiyo imeandaa mfumo mbadala, alioutaja kuwa ni Spreadsheet Excel RMS, ambao utatumika iwapo kutakuwa na changamoto katika kutumia mfumo uliondaliwa. Aidha alisema tume hiyo inafanya maandalizi ya kutumia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa ajili ya kutuma matokeo yote, badala ya kutumia mtandao wa simu za mkononi. “Katika uchaguzi wa mwaka 2010, utumaji wa matokeo ulikuwa na changamoto nyingi. Kati ya majimbo 239 ni majimbo 150 tu yaliweza kutuma matokeo kwa mfumo uliokuwa umeandaliwa, ambao ni kupitia mtandao wa simu za mikononi, matokeo yaliyobaki yalitumwa kwa nukushi ,” alifafanua. Alisema kitendo cha kutumia mkongo huo wa taifa, kitasaidia upatikanaji wa matokeo mapema kama inavyokusudiwa, ingawa pia njia mbadala ya kutuma matokeo kwa nukushi imeandaliwa na halmashauri zote zimepatiwa vifaa, vitakavyowezesha utumaji wa matokeo kwa haraka kufanyika. Aidha, tume imekubaliana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kuhusu kutumia Mkongo wa Mawasiliano wa Tamisemi, kusaidia utumaji wa taarifa za matokeo kutoka katika halmashauri hadi NEC. Kuhusu elimu, Kombwey alisema jumla ya asasi za kiraia 451 ziliomba kutoa elimu ya mpiga kura. Kati ya hizo ni asasi 447 zilikidhi vigezo na hivyo kupewa kibali cha kutoa elimu hiyo. Alisema asasi hizo zimesaini Maadili ya Utoaji wa elimu ya Mpiga kura na kukubali kutumia mwongozo wa Elimu ya Mpiga kura.

DR Mtikila Aliuawa Kabla ya Ajali....DP

DR Mtikila Aliuawa Kabla ya Ajali....DP MAPYAA! Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrati (DP), Abdul Juma Mluya ameibuka na kusema mazingira ya kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Mchungaji Christopher Mtikila yamejaa utata huku akiweka wazi kwamba, inavyoonekana aliuawa kabla ya ajali yenyewe. Mtikila alifariki dunia katika ajali ya gari aina ya Toyota Corolla namba T189 ARG, Oktoba 4, 2015 iliyotokea kwenye Kijiji cha Msolwa, Bagamoyo, Pwani. Wengine watatu walijeruhiwa. mtikila2 Mti ambao gari liliugonga kwa juu kabla ya kupinduka. Akizungumza na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye ofisi ndogo ya chama hicho nyumbani kwa marehemu, Mikocheni B jijini Dar, Mluya alisema hata watu waongee vipi, lakini uchunguzi wao umeonesha kwamba, kiongozi wao aliuawa tofauti na eneo la ajali na mwili kwenda kutupwa pale. ROHO YAKE ILIWINDWA KWA SIKU 40 Mluya alisema: “Ndugu mwandishi, Mchungaji Mtikila kama kufa alikuwa afe muda mrefu sana pengine siku arobaini zilizopita (mpaka siku ya kifo cha kweli), kwa sababu amewindwa na watu ambao hatujajua lengo lao kubwa lilikuwa nini! “Kila alikokwenda kwa shughuli za kichama kulikuwa na timu ya watu inayomfuatilia.” mtikila4 ...Baada ya Kupinduka MARA YA KWANZA “Tarehe siikumbuki, lakini ni Septemba mwanzoni. Tulikuwa Bunda, Mara kwenye shughuli za chama, kuna watu ambao walikuwa hawaeleweki walitufuata mpaka hotelini. “Baada ya kubaini hilo, nilimuuliza mwenyekiti kuhusu ratiba aliyokuwa nayo ya kuzungumza kwenye runinga ya Staa TV. “Alinipa ratiba. Baada ya kumaliza kuzungumza, nilimwambia Bunda si mahali pa kulala hivyo nilimshauri aondoke, aende Mwanza. Na nilimwambia dereva wake aondoke bila kuaga.” mtikila4 (2) WAKIWA NJIANI “Lakini cha ajabu, wakiwa njiani wakielekea Mwanza kuna gari liliwafuata kwa nyuma kwa mwendo ambao waliutulia shaka. Dereva wa mwenyekiti alipokuwa akiongeza mwendo, naye anaongeza, akipunguza naye anapunguza. “Ilibidi dereva amwambie mwenyekiti naye akamtaka dereva aongeze kasi hadi Mwanza.” “Katika ratiba yetu tulitaka kufanya ziara za kichama kuanzia Oktoba 18, mwaka huu kwa kuanzia mkoa wa Kigoma na kwingineko. Pamoja na kufuatiliwa kote kule mwenyekiti hakuwa na roho ya uoga hata kidogo. Alimtanguliza sana Mungu. “Kwa hiyo wasiwasi mkubwa wa kufuatiliwa na watu hao ulianza Mara na Mwanza kwa nyakati tofauti. “Septemba 11, mwaka huu ndiyo tarehe ambayo sasa nilianza kukariri matukio hayo hatua kwa hatua. Siku hiyo tulikwenda kwenye Kijiji cha Usangu mkoani Pwani kwa ajili ya kufanya kampeni ya mgombea udiwani. Baada ya kumaliza tuliamua kurudi Dar lakini njiani dereva akasema kuna watu hawajui wanakuja nyuma yetu.” WAPOTEA NJIA KWA KUFUATILIWA “Tulijikuta tukipotea njia na kutokea mjini Kisarawe (Pwani). Pale tulifika kituo cha mafuta ambapo tulikuta gari aina Toyota Land Cruiser VX limepaki kama vile ni watu pia walikuwa wakitufuatilia. “Lengo la kusimama pale lilikuwa kupata chakula lakini hatukufanya hivyo kulingana na mazingira. Tukaanza safari ya kurudi Dar. Tulipofika Pugu Sekondari, gari lile lilitupita kwa kasi na kupotea. “Tulipofika Tazara gari lile lilionekana na wakati huo yalikuwa mawili. Kilichotushangaza ni upya wa magari lakini eti namba zinaanzia na A. Mimi nilifikiria kwamba, pengine ni za idara ya usalama wa taifa zilikuwa doria mbalimbali hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi. “Ndugu mwandishi, mimi ninafanya kazi ya siasa, niko makini sana. Niliwaambia wenzangu kuwa tunafuatiliwa. “Ndani ya gari sisi tulikuwa na viongozi wa kuwapeleka Temeke. Lakini baada ya kufika huko lile VX tulikutana nalo. Tulipomuacha yule tuliyempeleka kule, tukawa tunampeleka mchungaji nyumbani kwake (Mikocheni) lakini bado lile gari lilikuwa likitufuatilia.” WAPIGA CHENGA “Tulipofika maeneo ya Msasani kwa Mwalimu (Julius Nyerere) dereva alikunja kona kuelekea kwa mchungaji na lile gari likakunja kona na kurudi lilikotoka.” SIKU NYINGINE “Siku iliyofuata tulipanga mipango yote ambapo sasa tulisema Oktoba 18, mwezi huu tuanze ziara ya mkoa wa Kigoma na maeneo mengine ya Kanda ya Ziwa. “Mimi niliondoka kuelekea Shinyanga, yeye (Mchungaji) aliandaa safari ya kwenda Njombe kwenye kampeni ya mgombea Ubunge Jimbo la Njombe.” OKTOBA 2, 3, 2015 “Mwenyekiti aliondoka Dar Oktoba 2, kuelekea Njombe. Oktoba 3, alinipigia simu asubuhi na kunijulisha kuwa jana yake walipata ajali maeneo ya Makambako wakati wanakwenda. “Nilimuuliza alipata matibabu, akajibu kuna viongozi wa Njombe walifika na kumchukua hivyo yuko sawasawa.” TAARIFA YA AJALI “Siku hiyo hiyo walifanya kampeni na jioni yake walianza safari ya kurejea Dar. Walipofika Mkoa wa Pwani, saa kumi na moja alfajiri, Mchungaji Mgaya alinipigia simu na kuniambia walikuwa njiani wanarudi Dar, wamepata ajali mbaya sana. Lakini hakuniambia kama mchungaji amefariki dunia. “Nilianza kufuatilia tukio hilo na kuuliza kama kuna msaada wowote wameupata, akasema mpaka muda huo polisi walikuwa hawajafika. Mimi napenda sana kufungua mitandao ya kijamii, nilipofungua nikakuta picha zilishasambaa kwenye mitandao kitu ambacho nilijiuliza usiku huo huyo mpigapicha alikuwa wapi?” SHAKA KUBWA YA DP “Sisi DP, mashaka yetu makubwa ni mazingira mazima ya namna kiongozi huyo alivyofariki dunia. Hata mtoto hawezi kudanganywa kwa namna hiyo. DP ina taasisi ya kufanya uchunguzi iitwayo Liberty International Foundation iliyokuwa ikisimamiwa na marehemu. Ipo kazini kwa sasa ili kubaini ukweli wa kifo cha mwenyekiti na tutaweka wazi kila kitu.” “Laini pia tunaitaka serikali kufanya uchunguzi na kutoa taarifa hadharani.” MWENYEKITI KIJIJI AIBUKA NA YAKE Uwazi pia lilifika aneo la ajali na kujionea kwa macho mazingira yake na kupata maelezo kutoka kwa baadhi ya mashuhuda. Joshua Mohamed Msigala ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Msolwa, Chalinze, Pwani palipotokea ajali. Yeye anasimulia mambo aliyoelezwa na mmoja wa majeruhi, Mchungaji Patrick Mgaya siku ya tukio. “Kwanza kabisa waandishi wa habari mmefanya vizuri kufika eneo la tukio na kujionea hali halisi. Nawaeleza hali halisi ilivyokuwa mpaka mimi kufika eneo la ajali. “Siku hiyo asubuhi ya saa kumi na moja na nusu kama sikosei, nikiwa nyumbani nilipigiwa simu na dereva mmoja wa lori anayenijua. Akasema ameona ajali maeneo yangu lakini hajui kama kuna waliokufa au la!” MWENYEKITI AWAHI NA BODABODA “Kusikia hivyo, nilichukua bodaboda ili niwahi. Nilifika ndani ya dakika kama kumi tangu kutokea kwa ajali. Nilikuta mwili wa Mtikila umelala pembeni ya gari huku wengine watatu waliodai walikuwa ndani ya gari wakiwa wamesimama tu. “Ila kati ya hao watatu, mmoja alijitambulisha kuwa ni Mchungaji Mgaya, yeye wakati nafika alikuwa akiongea kwa simu.” ALICHOAMBIWA NA MCHUNGAJI “Nilimuuliza mchungaji ilikuwaje? Akasema wakati wanapata ajali hiyo, marehemu Mtikila na wengine wawili walichomoka ndani ya gari hali iliyosababisha kifo cha Mtikila. Hata hivyo, kwa upande wangu sikuamini kama wote walichomoka kutoka kwenye gari bali mazingira yalionesha walitoka wenyewe. “Mchungaji alizidi kuniambia kuwa, gari lilipaa juu zaidi ya futi kumi na kugonga mti kisha likapinduka na kulalia paa (kwenye Uwazi siku ya tukio, mchungaji alisema gari lilibiringika). “Lakini pia siamini, kwani pamoja na kuona alama katika mti sikubali kama zilisababishwa na ajali kwani kama ni hivyo gari lingekuwa limepondeka zaidi juu lilikoangukia tofauti na lilivyokuwa likionekana.” KILICHOMSHANGAZA ZAIDI MWENYEKITI Mwenyekiti huyo alizidi kusimulia kushangaa kwake: “Kitu kingine kinachonishangaza ni kwamba, kwa maelezo yao gari liliacha barabara likawa linaendeshwa pembeni kwa umbali wa meta mia moja (urefu wa uwanja wa mpira). Kwa nini dereva asipunguze mwendo ambapo angefanya hivyo gari lisingefika kwenye mti.” “Kinachoshangaza kingine ni kwamba, hakuna majeraha yaliyoonekana kwa macho kwa walionusurika hata kuonesha kwamba walikatwa na vioo wakati wakirushwa nje kutoka ndani ya gari. Hata viti vya mbele vilikuwa vilevile, havikuharibika na kama majeruhi walirushwa nje walipitia wapi?” WALIOFIKA AWALI Mwenyekiti huyo alisema anawashukuru askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wa Kambi ya Kizuka na Sangasanga waliokuwa wakipita ambapo walifika kutoa msaada. “Baadaye mimi nilifanya mawasiliano na Polisi wa Kituo cha Chalinze (Bagamoyo) ambapo walifika eneo la tukio. Pia polisi wa mkoa nao walifika na saa 12:30 asubuhi majeruhi na mwili wa marehemu walipelekwa Hospitali Teule ya Rufaa Tumbi.” Naye Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Msolwa, Joseph Hamad kwa upande wake alisema alipokea taarifa saa 3 asubuhi na alipowasiliana na mwenyekiti alimwambia yupo katika eneo la tukio. Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho waliohojiwa na Uwazi walisema wameshangazwa na ajali hiyo iliyosababisha kifo cha Mchungaji Mtikila na kuitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina. SIMU YA MTIKILA YAZUA UTATA Mpaka tunakwenda mitamboni, familia ya Mtikila ilisema, jana ilitarajia kufuatilia simu ya marehemu kwani haijulikani ilipo na pia kujua walipo dereva (George Ponella) na msaidizi wake (Ally Mohamed) ambapo awali, dereva alishikiliwa na jeshi la polisi.

FLORA MBASHA Akiri..Mwanangu si wa Emmanuel Mbasha OHOOO!

FLORA MBASHA Akiri..Mwanangu si wa Emmanuel Mbasha OHOOO! Kimenuka tena. Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha amesema mwanaye mdogo (jina linahifadhiwa) hahusiani hata kidogo na aliyekuwa mumewe, Emmanuel Mbasha huku akidai kuwa anamtambua mwanaume huyo kama mzazi mwenzake kwa mtoto mmoja tu (Liz), Risasi Jumatano linakupa zaidi. Akizungumza na waandishi wetu kwa njia ya simu mwishoni mwa wiki, Flora alisema amechoshwa na manenomaneno yanayosemwa juu yake na Emmanuel na kwamba kama mumewe huyo ameamua kumwaga ugali, yeye yupo tayari kumwaga mboga. Mwimbaji huyo alisema kwamba kauli aliyoitoa hivi karibuni kuwa anampenda mumewe na kwamba yupo tayari kuishi naye haikutoka moyoni, isipokuwa alifanya hivyo kwa huruma tu, kwa sababu mwanaume huyo ni mtu katili, mwenye roho mbaya na asiyemuogopa Mungu. “Mtu mwenyewe alimtelekeza mtoto (Liz) kwa zaidi ya mwaka mmoja, ni mtu mbaya sana, sina mapenzi na Mbasha hata kidogo, ni afadhali niolewe na chizi anayeokota makopo kuliko kurudiana na mtu katili na mnyama kama huyo, namheshimu kama mzazi mwenzangu kwa Liz,” alisema. Mtoto anayedaiwa kuibua mazito. “Huyo mwanaume hafai kabisa, ni katili, namfananisha na shetani, anajifanya mwema kwa watu wakati hajawahi kuiomba msamaha familia, sikubaliani kabisa na hukumu ya mahakama, ukweli anaujua kwamba alibaka na hata mkimtaka huyo binti mumhoji nitamleta, isitoshe sasa hivi hata mtoto wake hamjali, hajui anasoma vipi, hajawahi kulipa hata shilingi ya ada, mimi mwenyewe ndo nahangaika kumlea mwanangu Liz ambaye anasoma kidato cha kwanza. “Hastahili kabisa kuitwa baba sababu mzazi mwenye akili hawezi kutelekeza familia hata kama tumegombana, nimemwachia nyumba niliyojenga kwa pesa yangu na pesa zote aliweka kwenye akaunti yake na zote nilimwachia lakini kashindwa kuihudumia familia.” Flora anajulikana kuwa na watoto wawili, mdogo akiwa ni yule aliyezaliwa wakati wanandoa hao wakiwa katika mzozo uliosababisha watengane hadi hivi sasa. Alipoulizwa kwa nini anadai aliyekuwa mumewe kumtelekeza mtoto mmoja tu, badala ya wawili, alifunguka. “Huyu mwanangu mdogo hausiki naye kabisa, tena asiwe anamtaja kabisa kwa sababu hamhusu, hajui hata matumizi yake yakoje, mengine kaka achana nayo tu,” alisema Flora. Mwimbaji huyo mwenye kipaji alipoulizwa sababu za kufuta kesi ya kudai talaka, aliyoifungua hivi karibuni katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati anadai hamtaki na hawezi kurudiana naye, alisema alifanya hivyo baada ya kushinikizwa na mtu ambaye hata hivyo, alikataa kumtaja. Mwimba Injili Bongo, Flora Mbasha.\ Flora alisema familia yake haijaridhishwa kabisa na suala la kesi ya ubakaji iliyokuwa ikimkabili mumewe kumalizika kwa kuachiwa huru na kwamba wanajipanga kwa ajili ya kukata rufaa.“Hiyo kesi imeisha kisiasa, Mbasha aliwahi kukiri kuwa ni kweli alifanya kitendo hicho, iweje leo aonekane hana hatia? Tutakwenda kukata rufaa ili haki itendeke.” Baada ya kuzungumza na Flora, mwandishi wetu alimtafuta Mbasha kwa lengo la kumuuliza kuhusu madai ya mtoto yule mdogo kutohusika naye kama alivyosema mkewe, naye bila ‘kutafuna maneno’, alisema hata yeye hamtambui huyo mtoto mdogo, ila anaomba arudishiwe mtoto wake mkubwa, Liz na maisha mengine yaendelee. “Hata mimi simtambui huyo mwingine, ninachoomba anirudishie tu mtoto wangu mkubwa Liz, huyo mwingine sihusiki naye kabisa kama alivyosema, yeye (Flora) ndiye anajua mhusika wa huyo mtoto, lakini si mimi na wala hajakosea kusema hivyo, nililitambua hilo tangu zamani, anipe tu mwanangu wa kwanza,” alisema Mbasha.

Diamond Opens Up About How Fathering Princess Tiffah Has Changed Him

Diamond and Zari Hassan’s daughter, Latiffah Nasibu Abdul aka Princess Tiffah has not only made the Dangote’s a tight-knit family but also changed her father’s life in a big way. Speaking to Tanzania’s leading radio station, Clouds FM, the singer who just bagged three awards at the just concluded 2015 AFRIMMA awards, said that he has been trying to be conduct himself in a more disciplined manner as he would not like his daughter to see ratchet pictures of her father grinding on women because she would be saddened by them.

Sunday, October 11, 2015

HUDDAH MONROE TW3RKS!! AND POSES IN NUD3 PHOTOS......... WATCH THE VIDEO!!. When huddah she is in Lagos shared this image and tw3rking after taken shower!! watch the video below.... WATCH THE VIDEO BELOW HUDDAH TW3RKS.....

WATCH THE VIDEO WHATS DIAMOND SPENDING WITH HIS TEAM IN LONDON IT'S GOOD TIME ...... MUST WATCH. Watch the video whats Diamond spending with his team in london it's Good time .... must watch the video here!! WATCH THE VIDEO BELOW!!

-LOWASA ATUA MUSOMA KWA KISHINDO


Nimekuwekea matukio ya kwanza kabisa ya Mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania CHADEMA MH EDWARD LOWASA wakati akiwasili musoma leo.picha zote zitakujia baadae 

Chama chochote cha siasa huzaliwa, hukua, kufikia kikomo, huzeeka na kufa kinaposhindwa kukabiliana na changamoto za wakati ule. Dalili za chama kuugua na kufa ni viongozi wake kupuuza haki za binadamu, kutoshughulikia kero za wananchi, kutumia ubabe na vitisho kuzima matakwa ya wananchi kama ilivyo sasa kwa CCM.

Hadi mwaka 1990 CCM ilikuwa chama cha wakulima na wafanyakazi lakini tangu kulipozinduliwa Azimio la Zanzibar CCM kimekuwa kikipata wakati mgumu. Kutokana na kushindwa kutimiza ahadi zake na kutokuwa karibu na wananchi, viongozi wake sasa wanaona aibu hata kusema 'CHAGUA CCM 'bali wanapiga kampeni kwa kusema 'CHAGUA MAGUFULI 'kana kwamba Magufuli ni mgombea binafsi.

Bahati mbaya kwa CCM badala ya kueleza watawafanyia nini wananchi wanatumia muda mwingi kufanya maigizo majukwaani na kutoa lugha za matusi na tuhuma ambazo wapinzani wanazipinga kwa hoja. Duniani kote, kazi ya chama makini cha upinzani ni kupinga sera mbovu za chama tawala na siyo kusifu.

Hofu ya CCM kuondolewa madarakani ipo dhahiri baada ya wananchi walio wengi kuelewa sera za wapinzani na kuziamini. Zimebaki siku 19 kabla ya uchaguzi tusubiri 25.10.2015 CCM itapoondoka madarakani .

#mabadiliko kwanza, kazi achia Punda.

Kama Mzee #Kingunge mwenye kadi namba 8 anataka #mabadiliko sasa wewe mwenye kadi 163837 unasubiri nini?

Ule usemi wa Mwanaume ni Mwanaume tu, Umetimia leo baada ya Makeke yote na Mbwembwe zote za Flora Mbasha Kumuishia na Kujikuta amekua mdogo kama piriton mbele ya Mumewe.

Nikakumbuka ule usemi wa Baba na Mama wakigombana Nyumbani, Waache wenyewe Mwisho wataelewana.

Wakati alipokua anahojiwa na Millad Ayo, Flora Mbasha kasema; "Yule ni mume wangu na bado nampenda na ntaendelea kumpenda. Tuna watoto wawili na ningependa tuongeze watoto mapacha lakini tusubili uchaguzi Uishe. Nlikua nampenda mume wangu sana ndo maana pete naivaa shingoni hii ndoa yangu na Mume wangu naipenda sana. Naomba anisamehe kwani nmeshamsamehe pia

Nipo na amani tele na namshukuru Mungu.

Namuahidi ntaendelea kumpenda siku zote. Ninachomuomba naye anisamehe" amesema Flora.

Mbasha mwenyewe kasema Kibiblia hakuna kuachana. Alikua natuma watu wamuombee Msamaha ili Flora arudi nyumbani walee watoto.

"Asisikilize watu na watu wanaompamba, Naomba arudi nyumbani" alinukuliwa Mbasha.


Lakini Baada ya mke wake kufuta kesi mahakamani na kufuta kesi ya kudai talaka, na Kumpigia Magoti Mumewe, Mume amegoma tena, amesema hamuhitaji tena. Kabadilisha maamuzi.

Rihanna anasema yeye ni kama wanawake wengine kiasi cha kuwa na hamu ya kufanya mapenzi na kwamba hajavunja amri ya sita kwa muda mrefu sasa.

rihanna-cover

Akiongea kwenye jarida la Vanity Fair, Rihanna alisema hawezi tu kufanya mapenzi na mtu ambaye hajamuingia moyo.

Haya ndio aliyoyasema:

If I wanted to I would completely do that. I am going to do what makes me feel happy, what I feel like doing. But that would be empty for me; that to me is a hollow move. I would wake up the next day feeling like s–t,” she shared. “That’s why I haven’t been having sex or even really seeing anybody. Because I don’t want to wake up the next day feeling guilty. I mean I get horny, I’m human, I’m a woman, I want to have sex. But what am I going to do—just find the first random cute dude that I think is going to be a great ride for the night and then tomorrow I wake up feeling empty and hollow? He has a great story and I’m like … what am I doing? I can’t do it to myself. I cannot. It has a little bit to do with fame and a lot to do with the woman that I am. And that saves me.

Kwenye mahojiano hayo pia, Rihanna alizungumza uhusiano wake na Chris Brown. “Nilikuwa msichana yule,” alisema Rihanna kueleza kwanini alimrudia Chris Brown licha ya kumjeruhi vibaya mwaka 2009.

Msichana yule aliyehisi maumivu makali kama uhusiano huu ulivyokuwa, pengine watu wengine wameumbwa kuwa na nguvu kuliko wengine. Pengine mimi ni miongoni mwa wale watu ambao wameumbwa kumudu mambo kama haya. Pengine mimi ni mtu ambaye ni kama malaika wa ulinzi kwa mtu huyu, kuwepo pale wanapokuwa hawajiwezi, pale wanaposhindwa kuielewa dunia, pindi wanapohitaji tu mtu wa kuwapa moyo katika njia chanya na kusema mambo sahihi.”

Rihanna anadai alidhani angembadilisha Breezy.

“Kwa asilimia mia. Nilikuwa nikimtetea sana,” alieleza Rihanna.

Nilihisi kwamba watu walikuwa hamwelewi. Lakini unajua, unagundua baada ya muda kuwa katika mazingira hayo wewe ndiye adui. Unataka mambo mema kwao, lakini unapowakumbusha kuhusu waliyokosea, ama kama ukiwakumbusha vipindi vibaya katika maisha yao, ama tu ukisema nipo tayari kuvumilia jambo fulani, hawakufirii – kwasababu wanajua haustahili kile wanachoenda kukupa.

Pamoja na hayo, Rihanna amesema hamchukii CB.

“Nitamjali mpaka siku nakufa. Sisi sio marafiki lakini si kwamba ni maadui. Hatuna uhusiano mkubwa sasa.”




Paul Makonda akizungumza katika mkutano wa kampeni wa Mgombea mweza wa Urais kupitia CCM Bi Samia Suluhu Hassan,mkoani Mwanza.

Makonda amesema kuwa hakuna uchanguzi mwepesi na raisi  kwa  CCM  kama wa mwaka huu

Kasema  mwaka  huu  CCM  inapambana  na  Vibaka,Wachochezi  na  Mafisadi  waliokimbilia  UKAWA.

Msikilize Makonda akizunngumza hapo chini


Thursday, February 19, 2015

Faiza Ally: Hapa Bongo Hakuna Staa Mwenye Figa Kali Kama yangu

Faiza Ally: Hapa Bongo Hakuna Staa Mwenye Figa Kali Kama yangu

Mzazi mwenziye na Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi aka Sugu Faiza Ally Amejigamba kwa kusema hapa Bongo hakuna staa yoyote Bongo mwenye figa kama yake ya kuweza kuvaa bikini na kujiachia kama yeye..Wengi wamejaa minyama nyama tu wakijiachia ni kichekesho ...Amesema ukitaka kujua wewe ni mrembo kiasi gani vaaa bikini na ujiachie......
Je Mdau kuna ukweli ?

Diamond Amnunulia Pete na Cheni za Gharama Mpenzi Wake Mpya Zari the Lady Boss

Diamond Amnunulia Pete na Cheni za Gharama Mpenzi Wake Mpya Zari the Lady Boss

Mapenzi Moto moto ya Mwanamuzi Diamond kwa Mpenzi wake mpya bado yanaendelea ku make headlines baada ya kumnunulia Pete na Cheni ya mkononi Zari the lady boss , Kama picha inavyoonyesha hapo zote ni za dhahabu pure ila gharama zake hatukuweza kujua kwa haraka ...

Zari Ameweka picha hiyo na kuandika maneno haya ..Woke up to some 24 carat eish. Thank you Boo, xoxo...#QueenTingz..

Wema Amuumbua Kajala!

Wema Amuumbua Kajala!


UBUYU: Gazeti la udaku la Amani, limeripoti kuwa mrembo na mwigizaji wa Bongo Movies ,Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amedaiwa kumuumbua shosti wake wa zamani, Kajala Masanja kwa kumwaga ‘ubuyu’ kwamba amefilisika baada ya kigogo maarufu kama CK anayedaiwa kuwa ndiye mpenzi wake, kuyumba kiuchumi.

Kigogo huyo aliyewahi kuwa na uhusiano na Wema kisha kumwagana naye, imedaiwa kuwa ile jeuri ya kununua magari ya kifahari, kumiliki biashara mbalimbali mjini, kwa sasa ameangukia pua kwani hawezi tena kujitutumua.

Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na Wema, baada ya kuhamishia majeshi kwa Kajala, Wema hakufurahia hivyo aliposikia uchumi umeyumba, amefurahia sana kufuatia ule msemo wa ‘adui muombee njaa.’

“Wema amefurahi sana, anawaambia marafiki zake kuwa malipo ni hapahapa duniani, Wema alimlipia Kajala dhamana ya sh mil. 13 ili asifungwe kwa msala wa kutakatisha fedha uliokuwa ukimkabili lakini akamgeuka na kumchukulia bwana wake, ule si ubinadamu kabisa,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, Kajala ana nuksi kwani CK alipokuwa na Wema alikuwa na mafanikio na kupata fedha kila kukicha lakini alipohamia kwa Kajala mambo ndiyo yakaharibika.
“Kajala ana nuksi, CK alipokuwa na Wema walikuwa wanapata fedha nyingi kila wakati lakini kwa Kajala wamefilisika kwelikweli,” kilisema chanzo na kuongeza:

“Madam mwenyewe amemshangaa sana CK kuishiwa fedha wakati alikuwa mtu wa kucheza na dola nyingi kila kukicha na aliwekeza fedha zake katika miradi mbalimbali.”

Jitihada za kumpata CK ili azungumzie ishu ya kuyumba kiuchumi hazikuzaa matunda lakini kwa mujibu wa mmoja wa watu ambao wanafanya naye kazi, kigogo huyo ameporomoka kiuchumi kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kufanya magumashi ya fedha kazini hadi kufikia hatua ya kutaka kufukuzwa kazi.

“CK hayuko vizuri kazini, ana majanga kibao, ile jeuri aliyokuwa akifanya na Wema na Kajala ilikuwa ni fedha za magumashi sasa kimemnukia kazini,” kilisema chanzo hicho ingawa mwenyewe alipotafutwa kwenye simu hakupatikana.
Wakati mwanahabari wa Amani akiendelea kuichimba habari hiyo, alifanikiwa kunasa ‘clip’ ya sauti ya Wema iliyoonesha dhahiri kwamba mrembo huyo amefurahishwa na kitendo cha wawili hao kukalia kuti kavu.

Sauti hiyo ya Wema inasikika akizungumza na shosti yake kumueleza jinsi gani Kajala ameumbuka maana alifikiri kutembea na shemeji yake ameula kumbe matokeo yake ameangukia pua kwani mwanaume amefilisika.“…Kajala sasa hivi anaendesha Noah (Toyota) ile yenye mastikamastika nakwambia…” ilisikika sehemu ya clip hiyo.

Paparazi wa Amaani alimvutia waya Wema ili aweze kufunguka zaidi kuhusiana na sakata hilo namna ambavyo amefurahia, simu yake iliita bila kupokelewa.Hata hivyo, mwandishi wetu alikwenda nyumbani kwake, mtaa wa Bwawani-Kijitonyama jijini Dar zaidi ya mara tatu kwa nyakati tofauti lakini hakufanikiwa kumpata baada ya mlinzi kudai amelala.

Mwanahabari wa Amani alimvutia waya Kajala ili kusikia naye anasemaje baada ya kudaiwa kuanguka kiuchumi, simu yake iliita bila kupokelewa lakini hata hivyo, rafiki yake wa karibu ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alikanusha madai ya kufilisika.“Kajala hajafilisika na hawezi kufilisika, hayo yatakuwa maneno ya watu tu,” alisema rafiki huyo wa Kajala.

Wema na Kajala waliwahi kuwa mashosti wa damu kabla ya kugombana ambapo chanzo kilitajwa kuwa ni CK,  mwaka jana walidaiwa kupatana lakini baadaye ikaelezwa kuwa bado wanaendeleza bifu.

Download Official Iyanya and Diamond Platnumz - Nakupenda (I Love You)

Download Official Iyanya and Diamond Platnumz - Nakupenda (I Love You)

Haya Sasa Huu ndio official Wimbo wa Diamond na Mwanamuziki Iyanya Kutoka Nigeria Unaoitwa Nakupenda (I love you ) Unaweza Kusikiliza ama Kuudownload Kupitia Link hiyo hapo chini ..
Kazi Kwako ..Usikilize alafu uniambie kama umekubamba ama la...... Huu Hapa: 

Ugaidi Tanga: Wasomali Wawili Watiwa Mbaroni

Ugaidi Tanga: Wasomali Wawili Watiwa Mbaroni


JESHI la Polisi nchini kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), limewatia mbaroni watuhumiwa wawili wanaodaiwa kuwa na asili ya Somalia katika msako unaoendelea dhidi ya kundi la wahalifu wa silaha mkoani Tanga.
 
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi mjini hapa, kimeiambia Mpekuzi kuwa watu hao walikamatwa jana saa 5 asubuhi katika eneo la Kijiji cha Amboni Mafuriko, baada ya kuonekana katika eneo hilo wakiwa wanashangaa na hawajui wanakokwenda.
 
Baada ya kuonekana kwa watu hao, wananchi wa kijiji hicho kilicho jirani na Kijiji cha Mleni ambako kundi la wahalifu wa silaha lilijificha, walitoa taarifa kwa polisi ambao walifika na kuwatia mbaroni.
 
“Ni kweli leo (jana) saa tano asubuhi huku eneo la Kijiji cha Amboni Mafuriko kuna watu wawili wenye asili ya Somalia walikamatwa baada ya wananchi kuwaona na kuwatilia shaka, na hivyo kufanikisha kukamatwa,” kilisema chanzo hicho.
 
Wakati huohuo, jeshi hilo linawashikilia watu wawili ambao ni wafanyabiashara na waumini wa dini ya Kiislamu wa Jumuiya ya Answar Suni mkoani hapa kwa tuhuma za kuhusishwa na tukio la kufadhili vikundi vya uporaji wa silaha dhidi ya polisi.
 
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, ndugu wa watuhumiwa hao walidai ndugu zao wamekamatwa na polisi siku tatu zilizopita.
 
“Kuna ndugu zetu wawili wameshikiliwa kwa mahojiano kwa zaidi ya siku tatu na hatujawahi kuwaona kila tukiwapelekea chakula na dhamana imekataliwa, hivyo hali hiyo inatupa wasiwasi mkubwa,”alisema mmoja wa ndugu wa watuhumiwa hao ambaye hakutaka jina lake litajwe.
 
Mbali na matukio ya kukamatwa watu hao, hali ya ulinzi katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo imeimarishwa, hasa katika wodi ambayo askari waliojeruhiwa kwenye tukio la Amboni wamelazwa wakiendelea na matibabu.
 
Mpekuzi  ilimpotafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fraser Kashai pamoja na Kamishna Mkuu wa Operesheni na Mafunzo nchini, Paul Chagonja, wote walisema wapo katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama. 

Mwanamke Amuua Mwanamke Mwenzake kwa Kummwagia Mafuta ya taa na Kumchoma Moto baada ya Kumfumania na Mumewe

Mwanamke Amuua Mwanamke Mwenzake kwa Kummwagia Mafuta ya taa na Kumchoma Moto baada ya Kumfumania na Mumewe


Mkazi wa kijiji cha Ibosa, kata ya Nyakato, Bukoba Vijijini, Amelia Richard (50) anatuhumiwa kumuua mwanamke mwenzake kwa kummwagia mafuta ya taa na kumchoma moto baada ya kumfumania na mumewe.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera,  Henry Mwaibambe  alitaja tukio hilo ni  la Februari 15, mwaka huu saa 3 usiku katika kijiji cha Ibosa kata ya Nyakata Bukoba vijijini.
 
Alimtaja aliyeuawa ni  Pelagia Martin (46) aliyeunguzwa mwili mzima. Kamanda alisema mwanamke huyo alicheleweshwa kufikishwa Hospitali ya Mkoa hadi kesho yake; Februari 16 baada ya wanafamilia kuomba wayamalize bila kwenda Polisi.
 
Makubaliano ya wanafamilia hao yalitokana na kile kilichoonekana kwamba  Amelia alimfumania Pelagia akiwa na mumewe,  Richard Bulebo (57) ndani ya nyumba yao.
 
Kwa mujibu wa Kamanda, Februari 16 walipoona hali ya majeruhi inazidi kuwa mbaya, ndipo walifika katika Kituo cha Polisi mjini Kati wakiomba msaada.
 
Polisi walimpeleka majeruhi huyo Hospitali ya Mkoa lakini alifariki kabla ya kupatiwa matibabu. Polisi inamshikilia Amelia na Bulebo kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.

Wednesday, February 18, 2015

Muuza Mishikaki Maarufu Temeke Stand Apata Kichapo Baada ya Kukutwa Anauza Mishikaki ya Nyama ya Paka

Muuza Mishikaki Maarufu Temeke Stand Apata Kichapo Baada ya Kukutwa Anauza Mishikaki ya Nyama ya Paka


Muuuza mishikaki maarufu temeke standi ya mabasi aitwaye Said mishikaki amekamatwa  na nyama ya paka jana akiwa anaitengeneza kwa ajili ya Kuchoma Mishikaki..
 
Wananchi wenye hasira kali walimshushia kipigo cha mbwa kwa hasira za kulishwa nyama ya paka bila kujua.

Picha za Uchi: Mpenzi wa Desire Luzinda akamatwa

Picha za Uchi: Mpenzi wa Desire Luzinda akamatwa


Franklin Emoubor, raia wa Nigerian ambaye alikuwa mpenzi wa mwanamuziki nyota wa kike nchini Uganda Desire Luzinda amekamatwa.

Waziri wa Maadili wa Uganda Mchungaji Simon Lokodo, amesema kuwa Mnaigeria huyo amekamatwa na kikosi cha polisi cha kimataifa cha Interpol.
  

Hata hivyo waziri huyo hakueleza iwapo Emoubor anayedaiwa kusambaza mtandaoni picha za utupu za Desire, amekamatwa akiwa wapi.

Fundi Saa Apokea Kichapo kizito Akidaiwa Kumlawiti Mtoto jijini Arusha

Fundi Saa Apokea Kichapo kizito Akidaiwa Kumlawiti Mtoto jijini Arusha


Mwanaume  mmoja ambaye ni fundi saa maeneo ya Stendi Kuu jijini Arusha jana alipokea kipigo cha mbwa mwizi baada ya kudaiwa kumlawiti mwanafunzi wa kiume wa darasa la tatu wa shule moja jijini humo.

Kingwendu kugombea ubunge mwaka huu

Kingwendu kugombea ubunge mwaka huu


Mwigizaji mkongwe wa vichekesho hapa Bongo, Rashid Mwinshehe "Kingwendu", amesema anajiandaa Kugombea Ubunge 2015 Kupitia Chama ambacho amedai Kuwa anaona Kinapendwa na Watanzania wengi bila ya Kutaja Jina la Chama hicho wala Jimbo atakalogombea.
 
Wataalamu wa Masuala ya Kisiasa Nchini, wameitafsiri Kauli hiyo ya Kingwendu Kwa Mitazamo tofauti, huku Wengi Kati yao Wakisema Kuwa Upinzani Una Nguvu Kubwa hivi sasa hapa Nchini, hivyo Sio ajabu Kwamba yawezekana Msanii huyu amevutiwa na Kuamua Kujiunga na Chama fulani Cha Upinzani Ili aendeshe harakati za Ukombozi wa Taifa hili.
 
Akizungumza na Mwandishi wa Tanzania Daima, Kingwendu alisema,"Ninajiandaa Kugombea Ubunge 2015 Kupitia Chama ninachoona Kinapendwa na Watanzania wengi Kwenye Jimbo ambalo ntalitaja hapo baadae Wakati Utakapofika...

"Bado ninafanya Mazungumzo na Washauri wangu wa Karibu Kuhusiana na Swala, nadhani ntaliweka Wazi muda Ukifika..."

Kortini kwa tuhuma za kununua "Malaya wa Buguruni Rozana"

Kortini kwa tuhuma za kununua "Malaya wa Buguruni Rozana"


WATU wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Jiji kwa tuhuma za kununua machangudoa katika eneo la Buguruni Rozana jijini Dar es Salaam. Watuhumiwa hao waolifikishwa Jumanne ya wiki hii katika mahakama hiyo ni Antidius Severian (25), Yaham Mihamed (24), Ally Hassan (35) na Mohamed Hamis (27).
  
Wakisomewa mashtaka na wakili wa Serikali, Ramadhan Kalinga mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Bernard Mpepo, alidai kuwa Februari 14, mwaka huu katika eneo la Buguruni Rozana watuhumiwa hao walikamatwa na askari mwenye namba E.7882D/CPL wakifanya manunuzi ya madada poa hao huku wakijua ni kosa kisheria.
 
Hata hivyo, washtakiwa hao walikana kosa hilo, ambapo Hakimu Mpepo, alisema dhamana kwa watuhumiwa hao ipo wazi ambapo aliwataka kila mmoja kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja atasaini dhamana ya Sh 200,000.
 
Watuhumiwa hao walishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi Februari 24, mwaka huu kesi itakapotajwa tena.

Balaa la Mchepuko: Mume wa mtu Aumbuka......Baada ya fumanizi Apewa kichapo kizito na kutembezwa Uchi

Balaa la Mchepuko: Mume wa mtu Aumbuka......Baada ya fumanizi Apewa kichapo kizito na kutembezwa Uchi


Mwanaume aliyetambulika kwa jina moja la Joseph amejikuta akiaibika vikali kufuatia kudaiwa kunaswa akiwa na mwanamke mwingine ilhali yeye ni mume wa mwanamke aitwaye Sophia.

Kwa mujibu wa mashuhuda, aibu hiyo ilimkuta Joseph, Februari 14, mwaka huu (Siku ya Wapendanao Duniani) kwenye Kitongoji cha Nyihongo wilayani Kahama, Shinyanga wakati wadau mbalimbali walikuwa kila mtu na wake.
 
Mashuhuda waliliambia Amani kwamba, Joseph ni fundi ujenzi na siku ya tukio alinaswa kwenye nyumba inayojengwa na yeye lakini ikiwa bado kumalizika.
  

“Jamaa mwenye mke alishajua kuwa Jose anamlia mali zake lakini akavumilia sana. Hakutaka kumuuliza Jose wala mke wake, yeye alitaka amfumanie laivu mwenyewe,” alisema shuhuda.

“Sasa siku ya tukio, Jose alionwa na mtu mmoja akiingia kwenye nyumba inayojengwa. Yule mtu alishajua Jose anachepuka na yule mke wa jamaa, akaenda kumwambia ndiyo wakamzukia na kumnasa,”kilisema chanzo.
 
Chanzo kikaendelea kuweka wazi kuwa, baada ya Jose kunaswa alitembezewa kichapo kizito na kupelekwa kwenye ofisi za serikali ya mtaa ambapo Jose alipigwa faini ya shilingi laki tatu.
 
“Lakini kilichotokea sasa ni kwamba, baada ya kulipa faini hiyo, mke wa Jose naye kwa hasira aliamua kuondoka nyumbani na kwenda kwao.
Mke wa aliyefumaniwa
“Alisema amelazimika kuondoka kwa Jose kwa sababu kitendo alichokifanya kimemtia aibu kubwa. Kwamba haiwezekani yeye atulie nyumbani Siku ya Wapendanao halafu mumewe akachepuke mitaani na mwanamke mwingine,” kilisema chanzo.

Lady Jaydee: Sina mtoto wala watoto, Sijawahi toa Kizazi ili Nifanikiwe Kifedha

Lady Jaydee: Sina mtoto wala watoto, Sijawahi toa Kizazi ili Nifanikiwe Kifedha


Lady Jaydee ameendelea kujibu maswali ya mashabiki wake kupitia Instagram, na maswali mengine aliyokutana nayo ni kuhusu kama ana mtoto au ameasili mtoto ambaye huonekana kwenye kipindi chake cha ‘Diary Ya LadyJaydee’ kinachorushwa kupitia EATV.

SWALI: Una watoto wangapi?
JIBU : Sina mtoto wala watoto 
 
SWALI: Utazaa lini?
JIBU : Sijajua mpk sasa nitazaa lini, ila siku yoyote ile ikitokea naweza kuzaa 
 
SWALI: Kwanini huna mtoto /watoto?
JIBU : Sina mtoto /watoto sababu sijawapata, nikipata nitakuwa nao. 
 
SWALI: Tunaskia ume adopt mtoto ? Na mtoto tunaekuona nae ni wa nani?
JIBU : Sija adopt mtoto, mtoto mnae muona ana shine like a star, ananiita Shangazi, ninaishi nae sbb ya ukaribu wa shule anayosoma ,Tunaishi wawili tu, mimi na yeye
Anaitwa “Mokonyo Yvonne Mbibo” Ni binti wa mdogo wangu @dabomtanzania 
 
SWALI: Tunaskia una mtoto mkubwa ulimzaa ukamuacha kijijini Shinyanga /Musoma
JIBU : Sina mtoto niliemuacha kijijini, sijawahi kuishi kijijini.
Sijawahi kuishi Musoma, kwetu ni Bunda na huwa naenda ikitokea misiba kuzika, sijawahi kuishi huko zaidi hata ya miezi 2 Shinyanga niliozaliwa ni mjini
 
Nilihama Shinyanga, kuja Dar es salaam nikiwa na miaka 11
Sijawahi kurudi kuishi huko tena zaidi ya kwenda kusalimia. 
 
SWALI: Tunaskia huzai, ulitoa kizazi ili ufanikiwe kifedha?
JIBU : Sijatoa kizazi na sifanyi kitu chochote unusual ili kupata mafanikio
 
Angalizo : Mwenyezi Mungu hadhihakiwi, so stop calling me names. …….Kesho anaijua yeye, lolote pia linaweza kutokea. Accept me the way I am”

Send to me a message relating to this blog, comments, opinion, any information etc.......

Name

Email *

Message *