Hofu ya CCM kuondolewa madarakani ipo dhahiri baada ya wananchi kuelewa sera za wapinzani kuziamini
Chama chochote cha siasa huzaliwa, hukua, kufikia kikomo, huzeeka na kufa kinaposhindwa kukabiliana na changamoto za wakati ule. Dalili za chama kuugua na kufa ni viongozi wake kupuuza haki za binadamu, kutoshughulikia kero za wananchi, kutumia ubabe na vitisho kuzima matakwa ya wananchi kama ilivyo sasa kwa CCM.Hadi mwaka 1990 CCM ilikuwa chama cha wakulima na wafanyakazi lakini tangu kulipozinduliwa Azimio la Zanzibar CCM kimekuwa kikipata wakati mgumu. Kutokana na kushindwa kutimiza ahadi zake na kutokuwa karibu na wananchi, viongozi wake sasa wanaona aibu hata kusema 'CHAGUA CCM 'bali wanapiga kampeni kwa kusema 'CHAGUA MAGUFULI 'kana kwamba Magufuli ni mgombea binafsi.
Bahati mbaya kwa CCM badala ya kueleza watawafanyia nini wananchi wanatumia muda mwingi kufanya maigizo majukwaani na kutoa lugha za matusi na tuhuma ambazo wapinzani wanazipinga kwa hoja. Duniani kote, kazi ya chama makini cha upinzani ni kupinga sera mbovu za chama tawala na siyo kusifu.
Hofu ya CCM kuondolewa madarakani ipo dhahiri baada ya wananchi walio wengi kuelewa sera za wapinzani na kuziamini. Zimebaki siku 19 kabla ya uchaguzi tusubiri 25.10.2015 CCM itapoondoka madarakani .
#mabadiliko kwanza, kazi achia Punda.
Kama Mzee #Kingunge mwenye kadi namba 8 anataka #mabadiliko sasa wewe mwenye kadi 163837 unasubiri nini?
0 comments:
Post a Comment