YOU ARE IN GOOD HAND WITH OUR COMPANY

ENJOY OUR SERVICE DAILY...............

CALL: +255765257825

WE ARE NOW SHINYANGA......

PRAY HARD AND WORK HARD

DON'T MISS, MAKE YOUR LIFE BETTER VIA TDIS.....

INFORMATION TECHNOLOGY is no 1

HELPS YOUR BUSINESS...........

Thursday, February 19, 2015

Faiza Ally: Hapa Bongo Hakuna Staa Mwenye Figa Kali Kama yangu

Faiza Ally: Hapa Bongo Hakuna Staa Mwenye Figa Kali Kama yangu

Mzazi mwenziye na Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi aka Sugu Faiza Ally Amejigamba kwa kusema hapa Bongo hakuna staa yoyote Bongo mwenye figa kama yake ya kuweza kuvaa bikini na kujiachia kama yeye..Wengi wamejaa minyama nyama tu wakijiachia ni kichekesho ...Amesema ukitaka kujua wewe ni mrembo kiasi gani vaaa bikini na ujiachie......
Je Mdau kuna ukweli ?

Diamond Amnunulia Pete na Cheni za Gharama Mpenzi Wake Mpya Zari the Lady Boss

Diamond Amnunulia Pete na Cheni za Gharama Mpenzi Wake Mpya Zari the Lady Boss

Mapenzi Moto moto ya Mwanamuzi Diamond kwa Mpenzi wake mpya bado yanaendelea ku make headlines baada ya kumnunulia Pete na Cheni ya mkononi Zari the lady boss , Kama picha inavyoonyesha hapo zote ni za dhahabu pure ila gharama zake hatukuweza kujua kwa haraka ...

Zari Ameweka picha hiyo na kuandika maneno haya ..Woke up to some 24 carat eish. Thank you Boo, xoxo...#QueenTingz..

Wema Amuumbua Kajala!

Wema Amuumbua Kajala!


UBUYU: Gazeti la udaku la Amani, limeripoti kuwa mrembo na mwigizaji wa Bongo Movies ,Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amedaiwa kumuumbua shosti wake wa zamani, Kajala Masanja kwa kumwaga ‘ubuyu’ kwamba amefilisika baada ya kigogo maarufu kama CK anayedaiwa kuwa ndiye mpenzi wake, kuyumba kiuchumi.

Kigogo huyo aliyewahi kuwa na uhusiano na Wema kisha kumwagana naye, imedaiwa kuwa ile jeuri ya kununua magari ya kifahari, kumiliki biashara mbalimbali mjini, kwa sasa ameangukia pua kwani hawezi tena kujitutumua.

Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na Wema, baada ya kuhamishia majeshi kwa Kajala, Wema hakufurahia hivyo aliposikia uchumi umeyumba, amefurahia sana kufuatia ule msemo wa ‘adui muombee njaa.’

“Wema amefurahi sana, anawaambia marafiki zake kuwa malipo ni hapahapa duniani, Wema alimlipia Kajala dhamana ya sh mil. 13 ili asifungwe kwa msala wa kutakatisha fedha uliokuwa ukimkabili lakini akamgeuka na kumchukulia bwana wake, ule si ubinadamu kabisa,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, Kajala ana nuksi kwani CK alipokuwa na Wema alikuwa na mafanikio na kupata fedha kila kukicha lakini alipohamia kwa Kajala mambo ndiyo yakaharibika.
“Kajala ana nuksi, CK alipokuwa na Wema walikuwa wanapata fedha nyingi kila wakati lakini kwa Kajala wamefilisika kwelikweli,” kilisema chanzo na kuongeza:

“Madam mwenyewe amemshangaa sana CK kuishiwa fedha wakati alikuwa mtu wa kucheza na dola nyingi kila kukicha na aliwekeza fedha zake katika miradi mbalimbali.”

Jitihada za kumpata CK ili azungumzie ishu ya kuyumba kiuchumi hazikuzaa matunda lakini kwa mujibu wa mmoja wa watu ambao wanafanya naye kazi, kigogo huyo ameporomoka kiuchumi kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kufanya magumashi ya fedha kazini hadi kufikia hatua ya kutaka kufukuzwa kazi.

“CK hayuko vizuri kazini, ana majanga kibao, ile jeuri aliyokuwa akifanya na Wema na Kajala ilikuwa ni fedha za magumashi sasa kimemnukia kazini,” kilisema chanzo hicho ingawa mwenyewe alipotafutwa kwenye simu hakupatikana.
Wakati mwanahabari wa Amani akiendelea kuichimba habari hiyo, alifanikiwa kunasa ‘clip’ ya sauti ya Wema iliyoonesha dhahiri kwamba mrembo huyo amefurahishwa na kitendo cha wawili hao kukalia kuti kavu.

Sauti hiyo ya Wema inasikika akizungumza na shosti yake kumueleza jinsi gani Kajala ameumbuka maana alifikiri kutembea na shemeji yake ameula kumbe matokeo yake ameangukia pua kwani mwanaume amefilisika.“…Kajala sasa hivi anaendesha Noah (Toyota) ile yenye mastikamastika nakwambia…” ilisikika sehemu ya clip hiyo.

Paparazi wa Amaani alimvutia waya Wema ili aweze kufunguka zaidi kuhusiana na sakata hilo namna ambavyo amefurahia, simu yake iliita bila kupokelewa.Hata hivyo, mwandishi wetu alikwenda nyumbani kwake, mtaa wa Bwawani-Kijitonyama jijini Dar zaidi ya mara tatu kwa nyakati tofauti lakini hakufanikiwa kumpata baada ya mlinzi kudai amelala.

Mwanahabari wa Amani alimvutia waya Kajala ili kusikia naye anasemaje baada ya kudaiwa kuanguka kiuchumi, simu yake iliita bila kupokelewa lakini hata hivyo, rafiki yake wa karibu ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alikanusha madai ya kufilisika.“Kajala hajafilisika na hawezi kufilisika, hayo yatakuwa maneno ya watu tu,” alisema rafiki huyo wa Kajala.

Wema na Kajala waliwahi kuwa mashosti wa damu kabla ya kugombana ambapo chanzo kilitajwa kuwa ni CK,  mwaka jana walidaiwa kupatana lakini baadaye ikaelezwa kuwa bado wanaendeleza bifu.

Download Official Iyanya and Diamond Platnumz - Nakupenda (I Love You)

Download Official Iyanya and Diamond Platnumz - Nakupenda (I Love You)

Haya Sasa Huu ndio official Wimbo wa Diamond na Mwanamuziki Iyanya Kutoka Nigeria Unaoitwa Nakupenda (I love you ) Unaweza Kusikiliza ama Kuudownload Kupitia Link hiyo hapo chini ..
Kazi Kwako ..Usikilize alafu uniambie kama umekubamba ama la...... Huu Hapa: 

Ugaidi Tanga: Wasomali Wawili Watiwa Mbaroni

Ugaidi Tanga: Wasomali Wawili Watiwa Mbaroni


JESHI la Polisi nchini kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), limewatia mbaroni watuhumiwa wawili wanaodaiwa kuwa na asili ya Somalia katika msako unaoendelea dhidi ya kundi la wahalifu wa silaha mkoani Tanga.
 
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi mjini hapa, kimeiambia Mpekuzi kuwa watu hao walikamatwa jana saa 5 asubuhi katika eneo la Kijiji cha Amboni Mafuriko, baada ya kuonekana katika eneo hilo wakiwa wanashangaa na hawajui wanakokwenda.
 
Baada ya kuonekana kwa watu hao, wananchi wa kijiji hicho kilicho jirani na Kijiji cha Mleni ambako kundi la wahalifu wa silaha lilijificha, walitoa taarifa kwa polisi ambao walifika na kuwatia mbaroni.
 
“Ni kweli leo (jana) saa tano asubuhi huku eneo la Kijiji cha Amboni Mafuriko kuna watu wawili wenye asili ya Somalia walikamatwa baada ya wananchi kuwaona na kuwatilia shaka, na hivyo kufanikisha kukamatwa,” kilisema chanzo hicho.
 
Wakati huohuo, jeshi hilo linawashikilia watu wawili ambao ni wafanyabiashara na waumini wa dini ya Kiislamu wa Jumuiya ya Answar Suni mkoani hapa kwa tuhuma za kuhusishwa na tukio la kufadhili vikundi vya uporaji wa silaha dhidi ya polisi.
 
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, ndugu wa watuhumiwa hao walidai ndugu zao wamekamatwa na polisi siku tatu zilizopita.
 
“Kuna ndugu zetu wawili wameshikiliwa kwa mahojiano kwa zaidi ya siku tatu na hatujawahi kuwaona kila tukiwapelekea chakula na dhamana imekataliwa, hivyo hali hiyo inatupa wasiwasi mkubwa,”alisema mmoja wa ndugu wa watuhumiwa hao ambaye hakutaka jina lake litajwe.
 
Mbali na matukio ya kukamatwa watu hao, hali ya ulinzi katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo imeimarishwa, hasa katika wodi ambayo askari waliojeruhiwa kwenye tukio la Amboni wamelazwa wakiendelea na matibabu.
 
Mpekuzi  ilimpotafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fraser Kashai pamoja na Kamishna Mkuu wa Operesheni na Mafunzo nchini, Paul Chagonja, wote walisema wapo katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama. 

Mwanamke Amuua Mwanamke Mwenzake kwa Kummwagia Mafuta ya taa na Kumchoma Moto baada ya Kumfumania na Mumewe

Mwanamke Amuua Mwanamke Mwenzake kwa Kummwagia Mafuta ya taa na Kumchoma Moto baada ya Kumfumania na Mumewe


Mkazi wa kijiji cha Ibosa, kata ya Nyakato, Bukoba Vijijini, Amelia Richard (50) anatuhumiwa kumuua mwanamke mwenzake kwa kummwagia mafuta ya taa na kumchoma moto baada ya kumfumania na mumewe.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera,  Henry Mwaibambe  alitaja tukio hilo ni  la Februari 15, mwaka huu saa 3 usiku katika kijiji cha Ibosa kata ya Nyakata Bukoba vijijini.
 
Alimtaja aliyeuawa ni  Pelagia Martin (46) aliyeunguzwa mwili mzima. Kamanda alisema mwanamke huyo alicheleweshwa kufikishwa Hospitali ya Mkoa hadi kesho yake; Februari 16 baada ya wanafamilia kuomba wayamalize bila kwenda Polisi.
 
Makubaliano ya wanafamilia hao yalitokana na kile kilichoonekana kwamba  Amelia alimfumania Pelagia akiwa na mumewe,  Richard Bulebo (57) ndani ya nyumba yao.
 
Kwa mujibu wa Kamanda, Februari 16 walipoona hali ya majeruhi inazidi kuwa mbaya, ndipo walifika katika Kituo cha Polisi mjini Kati wakiomba msaada.
 
Polisi walimpeleka majeruhi huyo Hospitali ya Mkoa lakini alifariki kabla ya kupatiwa matibabu. Polisi inamshikilia Amelia na Bulebo kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.

Wednesday, February 18, 2015

Muuza Mishikaki Maarufu Temeke Stand Apata Kichapo Baada ya Kukutwa Anauza Mishikaki ya Nyama ya Paka

Muuza Mishikaki Maarufu Temeke Stand Apata Kichapo Baada ya Kukutwa Anauza Mishikaki ya Nyama ya Paka


Muuuza mishikaki maarufu temeke standi ya mabasi aitwaye Said mishikaki amekamatwa  na nyama ya paka jana akiwa anaitengeneza kwa ajili ya Kuchoma Mishikaki..
 
Wananchi wenye hasira kali walimshushia kipigo cha mbwa kwa hasira za kulishwa nyama ya paka bila kujua.

Picha za Uchi: Mpenzi wa Desire Luzinda akamatwa

Picha za Uchi: Mpenzi wa Desire Luzinda akamatwa


Franklin Emoubor, raia wa Nigerian ambaye alikuwa mpenzi wa mwanamuziki nyota wa kike nchini Uganda Desire Luzinda amekamatwa.

Waziri wa Maadili wa Uganda Mchungaji Simon Lokodo, amesema kuwa Mnaigeria huyo amekamatwa na kikosi cha polisi cha kimataifa cha Interpol.
  

Hata hivyo waziri huyo hakueleza iwapo Emoubor anayedaiwa kusambaza mtandaoni picha za utupu za Desire, amekamatwa akiwa wapi.

Fundi Saa Apokea Kichapo kizito Akidaiwa Kumlawiti Mtoto jijini Arusha

Fundi Saa Apokea Kichapo kizito Akidaiwa Kumlawiti Mtoto jijini Arusha


Mwanaume  mmoja ambaye ni fundi saa maeneo ya Stendi Kuu jijini Arusha jana alipokea kipigo cha mbwa mwizi baada ya kudaiwa kumlawiti mwanafunzi wa kiume wa darasa la tatu wa shule moja jijini humo.

Kingwendu kugombea ubunge mwaka huu

Kingwendu kugombea ubunge mwaka huu


Mwigizaji mkongwe wa vichekesho hapa Bongo, Rashid Mwinshehe "Kingwendu", amesema anajiandaa Kugombea Ubunge 2015 Kupitia Chama ambacho amedai Kuwa anaona Kinapendwa na Watanzania wengi bila ya Kutaja Jina la Chama hicho wala Jimbo atakalogombea.
 
Wataalamu wa Masuala ya Kisiasa Nchini, wameitafsiri Kauli hiyo ya Kingwendu Kwa Mitazamo tofauti, huku Wengi Kati yao Wakisema Kuwa Upinzani Una Nguvu Kubwa hivi sasa hapa Nchini, hivyo Sio ajabu Kwamba yawezekana Msanii huyu amevutiwa na Kuamua Kujiunga na Chama fulani Cha Upinzani Ili aendeshe harakati za Ukombozi wa Taifa hili.
 
Akizungumza na Mwandishi wa Tanzania Daima, Kingwendu alisema,"Ninajiandaa Kugombea Ubunge 2015 Kupitia Chama ninachoona Kinapendwa na Watanzania wengi Kwenye Jimbo ambalo ntalitaja hapo baadae Wakati Utakapofika...

"Bado ninafanya Mazungumzo na Washauri wangu wa Karibu Kuhusiana na Swala, nadhani ntaliweka Wazi muda Ukifika..."

Kortini kwa tuhuma za kununua "Malaya wa Buguruni Rozana"

Kortini kwa tuhuma za kununua "Malaya wa Buguruni Rozana"


WATU wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Jiji kwa tuhuma za kununua machangudoa katika eneo la Buguruni Rozana jijini Dar es Salaam. Watuhumiwa hao waolifikishwa Jumanne ya wiki hii katika mahakama hiyo ni Antidius Severian (25), Yaham Mihamed (24), Ally Hassan (35) na Mohamed Hamis (27).
  
Wakisomewa mashtaka na wakili wa Serikali, Ramadhan Kalinga mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Bernard Mpepo, alidai kuwa Februari 14, mwaka huu katika eneo la Buguruni Rozana watuhumiwa hao walikamatwa na askari mwenye namba E.7882D/CPL wakifanya manunuzi ya madada poa hao huku wakijua ni kosa kisheria.
 
Hata hivyo, washtakiwa hao walikana kosa hilo, ambapo Hakimu Mpepo, alisema dhamana kwa watuhumiwa hao ipo wazi ambapo aliwataka kila mmoja kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja atasaini dhamana ya Sh 200,000.
 
Watuhumiwa hao walishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi Februari 24, mwaka huu kesi itakapotajwa tena.

Balaa la Mchepuko: Mume wa mtu Aumbuka......Baada ya fumanizi Apewa kichapo kizito na kutembezwa Uchi

Balaa la Mchepuko: Mume wa mtu Aumbuka......Baada ya fumanizi Apewa kichapo kizito na kutembezwa Uchi


Mwanaume aliyetambulika kwa jina moja la Joseph amejikuta akiaibika vikali kufuatia kudaiwa kunaswa akiwa na mwanamke mwingine ilhali yeye ni mume wa mwanamke aitwaye Sophia.

Kwa mujibu wa mashuhuda, aibu hiyo ilimkuta Joseph, Februari 14, mwaka huu (Siku ya Wapendanao Duniani) kwenye Kitongoji cha Nyihongo wilayani Kahama, Shinyanga wakati wadau mbalimbali walikuwa kila mtu na wake.
 
Mashuhuda waliliambia Amani kwamba, Joseph ni fundi ujenzi na siku ya tukio alinaswa kwenye nyumba inayojengwa na yeye lakini ikiwa bado kumalizika.
  

“Jamaa mwenye mke alishajua kuwa Jose anamlia mali zake lakini akavumilia sana. Hakutaka kumuuliza Jose wala mke wake, yeye alitaka amfumanie laivu mwenyewe,” alisema shuhuda.

“Sasa siku ya tukio, Jose alionwa na mtu mmoja akiingia kwenye nyumba inayojengwa. Yule mtu alishajua Jose anachepuka na yule mke wa jamaa, akaenda kumwambia ndiyo wakamzukia na kumnasa,”kilisema chanzo.
 
Chanzo kikaendelea kuweka wazi kuwa, baada ya Jose kunaswa alitembezewa kichapo kizito na kupelekwa kwenye ofisi za serikali ya mtaa ambapo Jose alipigwa faini ya shilingi laki tatu.
 
“Lakini kilichotokea sasa ni kwamba, baada ya kulipa faini hiyo, mke wa Jose naye kwa hasira aliamua kuondoka nyumbani na kwenda kwao.
Mke wa aliyefumaniwa
“Alisema amelazimika kuondoka kwa Jose kwa sababu kitendo alichokifanya kimemtia aibu kubwa. Kwamba haiwezekani yeye atulie nyumbani Siku ya Wapendanao halafu mumewe akachepuke mitaani na mwanamke mwingine,” kilisema chanzo.

Lady Jaydee: Sina mtoto wala watoto, Sijawahi toa Kizazi ili Nifanikiwe Kifedha

Lady Jaydee: Sina mtoto wala watoto, Sijawahi toa Kizazi ili Nifanikiwe Kifedha


Lady Jaydee ameendelea kujibu maswali ya mashabiki wake kupitia Instagram, na maswali mengine aliyokutana nayo ni kuhusu kama ana mtoto au ameasili mtoto ambaye huonekana kwenye kipindi chake cha ‘Diary Ya LadyJaydee’ kinachorushwa kupitia EATV.

SWALI: Una watoto wangapi?
JIBU : Sina mtoto wala watoto 
 
SWALI: Utazaa lini?
JIBU : Sijajua mpk sasa nitazaa lini, ila siku yoyote ile ikitokea naweza kuzaa 
 
SWALI: Kwanini huna mtoto /watoto?
JIBU : Sina mtoto /watoto sababu sijawapata, nikipata nitakuwa nao. 
 
SWALI: Tunaskia ume adopt mtoto ? Na mtoto tunaekuona nae ni wa nani?
JIBU : Sija adopt mtoto, mtoto mnae muona ana shine like a star, ananiita Shangazi, ninaishi nae sbb ya ukaribu wa shule anayosoma ,Tunaishi wawili tu, mimi na yeye
Anaitwa “Mokonyo Yvonne Mbibo” Ni binti wa mdogo wangu @dabomtanzania 
 
SWALI: Tunaskia una mtoto mkubwa ulimzaa ukamuacha kijijini Shinyanga /Musoma
JIBU : Sina mtoto niliemuacha kijijini, sijawahi kuishi kijijini.
Sijawahi kuishi Musoma, kwetu ni Bunda na huwa naenda ikitokea misiba kuzika, sijawahi kuishi huko zaidi hata ya miezi 2 Shinyanga niliozaliwa ni mjini
 
Nilihama Shinyanga, kuja Dar es salaam nikiwa na miaka 11
Sijawahi kurudi kuishi huko tena zaidi ya kwenda kusalimia. 
 
SWALI: Tunaskia huzai, ulitoa kizazi ili ufanikiwe kifedha?
JIBU : Sijatoa kizazi na sifanyi kitu chochote unusual ili kupata mafanikio
 
Angalizo : Mwenyezi Mungu hadhihakiwi, so stop calling me names. …….Kesho anaijua yeye, lolote pia linaweza kutokea. Accept me the way I am”

Sunday, February 15, 2015

Sikiliza na Download Diamond Platnumz Ft. P-Square

Unaweza Kusikiliza ama Kudownload Wimbo mpya wa Diamond Featuring P-Square 

Mungu ni Mkubwa: Mama yake Diamond Arejeshwa toka India......Afya yake kwa sasa inatia Moyo

Mungu ni Mkubwa: Mama yake Diamond Arejeshwa toka India......Afya yake kwa sasa inatia Moyo


Mungu ni  mkubwa :Mama mzazi wa Supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’, amerejeshwa Bongo kutoka India ambapo afya yake imetengemaa.

Habari kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya familia ya jamaa huyo, kimesema kwamba tayari  Sandra amesharejea katika hali yake ya kawaida na ndiyo maana akarudi Bongo baada ya kulazwa hospitalini nchini India kwa kusumbuliwa na ugonjwa wa kupooza.
 
Mwanafamilia huyo alisema kwamba, Diamond na mama yake walirejea nchini wikiendi iliyopita baada ya kufanyiwa matibabu ya kina na madaktari kujiridhisha kwa hali ya juu dhidi ya afya yake ambapo waligundua hali aliyonayo kwa sasa imetengemaa hivyo wakamruhusu kurejea kuungana na familia yake.
 
Habari zilieleza kuwa kwa sasa bimkubwa huyo yupo fiti na anaendelea na mazoezi ya kawaida huku akimalizia dawa alizopewa na wataalam hao wa afya.

Mapambano Makali Bado Yanaendelea Kuwasaka MAGAIDI wa Tanga.....Hii ni Video ya Magaidi hao Wakijisifia

Mapambano Makali Bado Yanaendelea Kuwasaka MAGAIDI wa Tanga.....Hii ni Video ya Magaidi hao Wakijisifia


Kutokana na wahalifu wanaopambana  na polisi na Jeshi la Wananchi (JWTZ) kutokamatwa, hali ya wasiwasi imeendelea miongoni mwa wakazi wa mjini hapa.

Sasa wananchi hao wameiomba Polisi kutoa tamko, kuhusu kikundi kilichorushiana risasi na askari Polisi na kusababisha kifo cha mwanajeshi mmoja.
 
Aidha, wananchi  hao wameitaka Polisi kutoa ufafanuzi kuhusu mwendelezo wa matukio  mengi ya uhalifu wa kutumia silaha, ambayo bado hayajapatiwa ufumbuzi, ikiwemo kutokamatwa kwa watuhumiwa wa matukio hayo.
 
Hata hivyo, Msemaji wa Polisi, Advera, alisema Jeshi lake halina taarifa zaidi ya iliyotolewa juzi na Mkuu wa Opersheni wa jeshi hilo, Kamishna Paul  Chagonja.
 
Habari za kipolisi zinasema kwamba bado wanaendelea kusaka wahalifu hao huku baadhi ya vikosi vya ulinzi na usalama, vimeongezwa kwa ajili ya kupambana na wahalifu hao.
 
Juzi  Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Polisi walipambana na kundi la wahalifu katika maeneo ya mapango ya Amboni na kusababisha wanajeshi wanne na polisi wawili kujeruhiwa. Hata hivyo, kuna habari kuwa majeruhi mmoja  ambaye ni mwanajeshi alifariki baadaye akiwa hospitalini.
  
Habari zingine zinasema kwamba majeruhi wengine ambao ni polisi wanne na mwanajeshi mmoja, wanaendelea vizuri. 
  
Kuhusu mwanajeshi aliyekufa, polisi wamegoma kuzungumzia suala hilo, lakini habari zinasema aliyekufa ni mwanajeshi mwenye cheo cha sajenti.
 
Wananchi wametoa kauli hizo kwa nyakati tofauti jana, walipozungumzia tukio la juzi, lililosababisha mapigano ya kurushiana risasi baina ya askari na wahalifu,  wanaodaiwa kuficha silaha katika eneo la Mapango ya Amboni,  nje kidogo ya mji wa Tanga.
 
Walisema mpaka sasa bado hawajaridhishwa na mwenendo wa utendaji wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, pamoja na taarifa hafifu wanazotoa, kuhusu namna walivyoshughulikia tukio hilo la juzi kwenye mapango  hayo ya Amboni.
 
Ibrahim Mshote, mkazi wa Ngamiani Kati, alisema mbali na tukio la juzi, yapo matukio mengine yakiwamo yaliyosababisha mauaji kwa raia, ambao walivamiwa na kuporwa mali na watuhumiwa kushindwa kupatikana. 
  

Alisema  hakuna taarifa za mwendelezo wa kushughulikiwa kwa matukio hayo.
 
“Kwa mfano kuna  wananchi walilipuliwa na bomu la kutupwa kwa mkono wakati wakitazama mpira kwenye kibanda cha video hapo Amboni… pia yupo mfanyabiashara wa eneo la Mkumbara wilayani Korogwe ambaye hivi karibuni alivamiwa na kuuawa kwa risasi kabla ya kuporwa mali, pia tukio la utekaji wa gari eneo la Michungwani wilayani Handeni baada ya kuwekewa magogo barabarani”, alisema.
 
Aliongeza “Katika matukio kama hayo, tunaambiwa tu wahalifu hawakupatikana, upelelezi unaendelea, lakini ni zaidi ya wiki mbili sasa hakuna taarifa zozote zinazoonesha juhudi za mwendelezo wa kudhibiti wahalifu kama hao, badala yake matukio yameendelea kuongezeka”.
 
Miriam Jonas, mkazi wa Barabara ya Tano jijini Tanga, alisema kitendo cha askari kunyang’anywa silaha mbili za SMG zenye risasi 60 kwenye kibanda cha chipsi ni fedheha kwa kuwa vitendo hivyo vilishasahaulika mkoani hapa.
 
 “Tulitarajia wahusika wangekamatwa ndani ya muda mfupi, lakini wapi, Polisi hapa Tanga imeshindwa kabisa kutoa taarifa kuhusu tukio hilo hadi Kamishna Chagonja alipokuja na kuzungumzia tukio la juzi”,alisema.
 
Aidha, Mrisho Mashaka mkazi wa Kwaminchi alisema licha ya Chagonja kuwataka wakazi wa jiji la Tanga kutulia, kwakuwa hali ya usalama imeimarishwa, bado baadhi ya wananchi wanayo shaka na hofu kubwa kuhusu tamko hilo.
 
“Kinachoendelea kutupa hofu ni mgongano wa kauli za polisi kama tulivyosikia kwenye vyombo vya habari kwamba waliarifiwa kwamba silaha za moto zikiwemo walizoporwa askari Januari 26 zimefichwa ndani ya mapango, lakini kilichokutwa ni silaha za jadi yakiwemo mapanga, pinde na mishale na vifaa vya kutengeneza milipuko”, alidai.
 
Alisema vifaa vilivyotajwa kukutwa kwenye eneo la tukio ni tofauti  na madhara waliyopata askari, waliokuwa kwenye operesheni hiyo ya kusaka silaha hizo, ambayo yamesababisha kifo na majeraha makubwa kwa baadhi yao, ambao sasa wamelazwa kwenye Hospitali ya Mkoa ya Bombo.
 
“Binafsi bado napata kigugumizi kuelewa taarifa hii kwasababu bado inayo maswali mengi ya kujiuliza, je hao ni watu wa namna gani ambao wamefanikiwa kujeruhi vibaya askari na kisha kutoroka na silaha zilizokuwa zikitafutwa, wameelekea wapi? Je sisi tuko salama?”,alihoji.
 
Walidai vipo viashiria vinavyoonesha kwamba hali ya ulinzi na usalama mkoani hapa, haijatengemaa kutokana na hali ya mazingira iliyobainisha kwamba wahalifu hao waliweka makazi ndani ya mapango hayo bila kubainika mapema.
 
Mbali ya silaha za jadi, vitu vingine vilivyokutwa ndani ya mapango hayo ni pikipiki mbili, baiskeli tatu, mavazi ya aina mbalimbali na vyakula, ambavyo ni dhahiri vinaashiria kwamba watu hao walikuwa wakijipenyeza ndani ya jamii kutafuta huduma muhimu bila kufahamika kwamba ni wahalifu.
 
Aidha, walisema ripoti ya hivi karibuni ya hali ya uhalifu mkoani Tanga, ambayo ilitolewa na Kamanda  mwishoni mwa mwaka jana ilibainisha kuongezeka kwa makosa ya uhalifu, yanayofanywa dhidi ya binadamu kwa asilimia 2.11, ikilinganishwa na takwimu za makosa kama hayo yaliyoripotiwa mwaka 2013.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Frasser Kashai alibainisha hayo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu hali ya ulinzi na usalama mkoani humo kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Desemba mwaka jana.
 
Kamanda alisema kwamba mwaka 2014, makosa 7, 970 ndiyo yaliripotiwa kwenye vituo mbalimbali vya Polisi wilayani, ikilinganishwa na makosa 7,805 yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2013.
 
Wakazi hao wa Tanga walidai wanaamini kwamba takwimu hizo ni kiashiria tosha kwamba mambo hayako sawa, licha ya Kamishna Chagonja  kujitahidi kutoa matumaini.
 
Kutokana na mambo kama hayo, walisema kuna umuhimu mkubwa kwa jeshi hilo kujipanga kimkakati ili kuondoa tatizo hilo haraka kwasababu kila siku matukio mapya yanaibuka na watuhumiwa hawapatikani.

Hapo  chini  nimekuwekea  Video  nyingine  ya  Magaidi  wa  Tanga  Wakijigamba  kupora  Silaha:

Saturday, February 14, 2015

Le Mutuz Anatafuta Mke 'Kwa Kweli Nahitaji WIFE Baby U Know Nahitaji Bonge la Mke, Niombeeni '

Le Mutuz Anatafuta Mke 'Kwa Kweli Nahitaji WIFE Baby U Know Nahitaji Bonge la Mke, Niombeeni '

William Malecela Aka Lemutuz Ametangaza kuhitaji Mke katika Page yake ya Instagram huku akiomba watu wamuombee apate Bonge la Wife. lemutuz alipost picha akionyesha kitanda kikiwa hakija tandikwa na kuandika maneno haya hapa chini kama caption ya picha hiyo:

"kwa kweli nahitaji WIFE baby U know nahitaji bonge la mke hahahah people niombeeni basi nipate Le Wife U know this is not good yaani mpaka aje mfanyakazi je ukitokea moto hapa watu wakaingia wanakuta bed iko kwenye this mess U know jamani niombeeni nipate Le Wife hahahahahahah U know......Off to the Airport!, A-Town here I come leo DOWNTOWN KARATU LIVE! - le Mutuz

Friday, February 13, 2015

Rais Kikwete Afuta ADA ya shule za Sekondari Nchi Nzima

Rais Kikwete Afuta ADA ya shule za Sekondari Nchi Nzima

HATIMAYE Rais Jakaya Kikwete ametimiza ahadi yake aliyoitoa Agosti mwaka jana katika Chuo Kikuu cha Mzumbe cha Morogoro, kwamba amekusudia kufuta ada ya shule za sekondari nchi nzima.


Akizindua Sera mpya ya Elimu na Mafunzo 2014 katika Shule ya Sekondari ya Majani ya Chai, Kipawa jijini Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alitangaza kufutwa kwa ada ya sekondari, kuanzia mwakani.

Kwa tangazo hilo, Bajeti ya mwisho ya uongozi wa Rais Kikwete itakayoanza kujadiliwa Mei mwaka huu, itatakiwa kuwa na fungu la kulipa gharama ambazo wananchi wamekuwa wakitoa kwa watoto wao wanaosoma elimu ya sekondari katika shule za Serikali nchi nzima.

Kwa sasa wazazi wamekuwa wakilipa Sh 20,000 kwa shule za kutwa na Sh 70,000 kwa shule za bweni, ili watoto wao wapate elimu ya sekondari.

Ubora
Alisema sera hiyo imezingatia stadi za msingi ambazo ni kuandika, kusoma na kuhesabu, ili kuwezesha watoto kujengwa kwenye msingi mzuri na hata kwenye Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) hilo limezingatiwa.

“Hata kwenye mpango wa BRN tumelizungumza ili kuhakikisha inatolewa elimu bora. Tusifanye mambo ya kuchekesha mtoto anafika madarasa ya juu hajui kuandika, kusoma na kuhesabu.

 “Kuanzia sasa kama mtoto anafika darasa la pili, hajui kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK), ni bora asiende darasa la tatu…naamini watoto wakiimarishwa katika stadi za KKK itaondoa matatizo haya,” alisema.

Tathimini ya Msingi ya Taifa kwa ajili ya uwezo wa wanafunzi katika KKK, kwa wanafunzi wa Darasa la Pili iliyofanyika mwaka jana, ilibaini kuwa asilimia 98 ya wanafunzi wa Darasa la Pili nchini, walikuwa hawaelewi wanachokisoma.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alisema, tathimini hiyo imefanywa kwa baraka za Wizara yake kwa kushirikiana na Shirika la Misaada la Marekani (USAID), ili kupata taarifa kuhusu hali halisi ilivyo ya wanafunzi wa Tanzania kumudu stadi za KKK wanapofika Darasa la Pili.

Mafanikio
Mbali na mafanikio ya kufikia uwezo wa kuanza kutoa elimu ya msingi na sekondari bure, huku msisitizo ukiwekwa katika utoaji wa elimu bora, Rais Kikwete pia ilitangaza mafanikio mengine katika sekta ya elimu ambayo yamefikiwa katika uongozi wake wa miaka kumi.

Rais Kikwete alisema sasa elimu imepewa kipaumbele katika sera na shughuli za serikali, ndio maana Bajeti ya Elimu, ndio kubwa kuliko bajeti zote.

Alifafanua kuwa mwaka 2005/06 bajeti hiyo ilikuwa Sh bilioni 6.7, wakati mwaka huu wa fedha imepanda na kufikia Sh trilioni 3.1.

Hatua hiyo ya kibajeti kwa mujibu wa Rais Kikwete, ni ongezeko la mara tano ya Bajeti ya mwaka 2005 sawa na asilimia 20 ya Bajeti ya Serikali ambayo inatengwa kwa ajili ya elimu.

Katika suala la mikopo kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya juu, Rais Kikwete alisema imetoka Sh bilioni 56 kwa mwaka wa fedha 2005/06, hadi kufikia Sh bilioni 345 kwa mwaka huu wa fedha.

Aidha, kwa mwaka jana, wanafunzi wanaonufaika na mikopo ya elimu ya juu, waliongezeka kutoka wanafunzi 16,000 mwaka 2005 hadi kufikia 95,000.

Kwa upande wa shule za msingi, alisema zimeongezeka kutoka 14,000 kwa mwaka 2005 hadi kufikia shule 16,343 kwa mwaka 2014, huku shule za sekondari zikiongezeka kutoka 531 kwa mwaka 2005, hadi kufikia 4,576, mwaka 2014.

Idadi wanafunzi wanaojiunga na sekondari, Rais Kikwete alisema imeongezeka kutoka wanafunzi 524,325 mwaka 2005 na kufikia wanafunzi milioni 1.8.

Rais Kikwete alisema pia vyuo vya ufundi vimeongezeka kutoka vyuo 184 mwaka 2005 na kufikia vyuo 744 kwa mwaka 2014, huku vyuo vikuu vikiongezeka kutoka vyuo vikuu 26 mwaka 2005 na kufikia vyuo vikuu 50 kwa mwaka 2014.

Alikumbusha kuwa kama sio kuanzishwa kwa shule za kata, idadi ya wanafunzi pia isingeongezeka.

“Hali imebadilika, sasa wanafunzi wengi wanakwenda shule na vyuoni na suala la watoto na vijana kupata fursa ya kusoma, sio tatizo katika sekta ya elimu, sasa kinachotakiwa ni kuhakikisha inapatikana elimu bora kwa kuboresha mazingira ya elimu,” alisema Rais Kikwete.

Mashabiki wanahisi ujumbe huu wa Diamond ni dongo kwa Wema!

 

Diamond Platnumz anafahamika kwa kushow love kwa kazi za wasanii wenzake kwenye Instagram. Mmoja wa wasanii walionufaika na shavu lake ni Shilole ambaye anapromote kava la single yake mpya ‘Malele’.

Akiweka picha hiyo, Diamond aliandika:


“Moja ya mfano mzuri tulionao Nchini…wakati anaanza kila mtu alimdharau na kumuona hatofika popote laikini leo hii Huwezi kuskia show kubwa inafanyika Nchini bila yeye Kuwepo…Dada zangu msikubali kuishi maisha ya kutegemea, Mbona mkijiamini wenyewe mnaweza… hivi hadi lini mtanyanyasika na Kuporwaporwa vitu baada ya Mahusiano kufa..Amkeni sasa! #Sio_wanaake_wote Huu mzigo wake mpya #MALELE.”

Hata hivyo mashabiki waliipigia mstari sentensi hii: Dada zangu msikubali kuishi maisha ya kutegemea, mbona mkijiamini wenyewe mnaweza… hivi hadi lini mtanyanyasika na kuporwaporwa vitu baada ya mahusiano kufa..Amkeni sasa!
Asilimia kubwa ya watu waliocomment kwenye post hiyo wanaamini sentesi hiyo imemlenga ex wake, Wema Sepetu.
Hizi ni baadhi ya comments:
Rinahjoe: Be a man niqque!! u’ve started to be a hypocrite, n a clapp_trapp man. On the ada syd no man z insecure as u as far as I can tell!!! Y all those insecurities lol… Yew too much now #SMFH hop t ‘ll be sweet if u behave manly!!! #PPB @diamondplatnumz
mamshafm: @diamondplatnumz punguza uswahili huo wewe ni msanii mkubwa. Kama ni ushauri huu ungeutoa kipindi upo kwenye mahaba mazito na @wemasepetu. Au kipindi hicho hukuona juhudi za Shilole? Na je juhudi zake na kuhongwa then kunyang’anywa vitu kwa wanawake vinahusianaje na juhudi za Shilole? Kila mkiachana na Wema wewe ndiyo hua mropokaji ropokaji tu. si tayari upo na Zari sasa mbona chokochoko kwa Wema haziishi? Hebu kukua kwako kwa akili na fikra kuende sambamba na kukua kwako kimuziki. Shame on you.
chasek84: Kwa caption hii,leo ndio nimeamini mjomba umeachika,sasa cha kufanya jikaze kiume,maana huyo unayempiga vijembe ndio màma wa shemeji yako,na ndio mkwe wa dada yako,mapenzi yafe,lkn udugu ubaki,sasa siku dada akijifungua mkikutana hospital na x wako,mtakuwa hamsalimiani,pia mjomba ulifanya haraka kujitika yule bi mkubwa,wakati bado unampenda x wako,ugomvi wenu ulikuwa unazungumzika,unaona sasa badio anakujia ndotoni,tatizo nini mjomba,au ndio nyota,dah kweli nimeamini kuna xna kuzidisha,ndio basi tena.
fetty94: Duu @diamondplatnumz kweli ww unahitaji ndimu na malimao maana umeumia sana mwanaume unatabia za kike ukiekewa mume mwenzio na wema cndo utazimia kweli wa tandale watandale tu hata aishi wapi
fartoolarge: Kuporwaporwa vitu…. hivi kuna yule mpenzi wake diamond, alinyang’anywa gari na vitu vingine baada ya kurudiana na diamond.. nani sijui vile… (wamanyema tunaongea ila chibu kazidi,… vijembe 101)
meggieimpostra: Kweli kuachwa kubayaaa hpn chezeaa sbb anajiabisha @diamondplatnumz na maneno yake mengine anayoandika inaonkna dhahiri imemuuma sanaaa sasa angalia ukifanychoo ujiulizi mbnaa @wemasepetu aongei lolote juu yako anafnya yake kwani wadhani hana anayoyajua kwako au hn la kuongea akutaka tuu so jieshimu na isitoshe utachongaaa weee mwsho wa siku unarudi kwake acha kujiabishaaa we ni mwanaume kufa kiumee kuachwa kupo kuibiwa kupoo ila we uliebiwa unaypokeaje na ujue yule ni mremboo so fanya yakooo.

Send to me a message relating to this blog, comments, opinion, any information etc.......

Name

Email *

Message *