Mkuu wa Wilaya Awapiga Marufuku Waganga Watoa UCHAWI
MKUU wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Betty Mkwasa amepiga marufuku shughuli zote za waganga wa kutoa uchawi maarufu kama lambalamba.
Alisema sasa itaandaliwa amri halali na akisikia kijiji kina lambalamba, mtu wa kwanza kukamatwa ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji kwani inaonesha waganga hao wamekuwa na ushirikiano na viongozi hao.
Alitoa kauli hiyo juzi baada ya kutembelea kijiji cha Uhelela na kukuta lambalamba wamepiga kambi katika kijiji hicho baada ya wananchi kuchanga fedha za kuwaita waganga hao.
Alisema wananchi wamekuwa mstari wa mbele kubariki kazi za waganga hao jambo ambalo linakuwa ni gumu katika kuwadhibiti na kuwabaini wachukuliwe hatua.
“Sasa tunawashikilia waganga wawili na tutawafikisha mahakamani wakatafute sehemu nyingine ya kufanya utapeli wao lakini si Bahi,”alisema.
Alisema wananchi walikuwa wakihitaji waganga hao wawasaidie kutokana na mvua kutonyesha. “Nimeambiwa wameingia katika kijiji cha Uhelela kwa lengo la kusaidia kunyesha kwa mvua ni mambo ya kipuuzi kabisa,” alisema.
Alisema wananchi walikuwa wakihitaji waganga hao wawasaidie kutokana na mvua kutonyesha. “Nimeambiwa wameingia katika kijiji cha Uhelela kwa lengo la kusaidia kunyesha kwa mvua ni mambo ya kipuuzi kabisa,” alisema.
Alisema haoni sababu ya wananchi kuita waganga hao ilhali walishapigwa marufuku katika wilaya hiyo na mkoa wa Dodoma kwa ujumla kwani wamekuwa wakiibia wananchi kwa lengo la kutoa uchawi na kufanya wananchi kuendelea kuwa masikini.
“Muwe na hofu ya Mungu, unamvisha joho la Mungu mganga wa kienyeji mtu anaamua bora alale na njaa ili fedha ampe lambalamba, mimi ni mcha Mungu ni mtu ninayethamini maendeleo hasa elimu, sitakubali upuuzi wa kishirikina usogee katika wilaya,” alisema.
Pia aliwaagiza watendaji wa vijiji kuwabaini watu wote wanaotumia waganga hao na kukamatwa kwa waganga wote wanaofanya shughuli hizo. Alisema ushirikina umekuwa ukirudisha nyuma wananchi kiuchumi.
“Uhelela wamekaribisha lambalamba lakini ni kijiji ambacho kipo nyuma katika suala la ujenzi wa maabara na wamekuwa wakichangia hadi Sh 50,000 kwa kaya kuita lambalamba lakini ukiwaambia mchango wa maabara wamekuwa hawatoi,” alisema.
0 comments:
Post a Comment