Tuesday, February 10, 2015

Wastara Awacharukia Wanao Mtukana Mumewe Mitandaoni

Msanii mkongwe katika gemu la filamu Bongo, Wastara Juma ameapa kumshtaki mtu atakayemkamata kutokana na baadhi ya mashabiki kuwa na tabia ya kumtukana matusi ya nguoni mtandaoni huku wakimhusisha na marehemu mumewe, Sajuki.

Akizungumza na gazeti  la  Ijumaa, Wastara alisema anajisikia vibaya baadhi ya mashabiki wanavyomtukana kwenye mitandao ya kijamii jambo ambalo siyo zuri kwani wanaingilia maisha yake binafsi na kibaya zaidi wanamhusisha Sajuki.

 

“Ukweli sipendi kabisa na nitamshtaki mtu maana wananitengenezea chuki kwani wakati mwingine wananitukana, wanamtukana sana Bondi huku wakidai kwamba nilikuwa naomba Sajuki afe ndiyo nifanye mabaya sasa sijui nimefanya kitu gani kibaya, kuwa na Bondi nimekuwa naye baada ya mume wangu kufariki maana mimi ni binadamu na kama angekuwepo nisingekuwa na mwanaume mwingine zaidi yake,” alisema Wastara.

0 comments:

Post a Comment

Send to me a message relating to this blog, comments, opinion, any information etc.......

Name

Email *

Message *